Baadhi ya wanawake wakimpokea Lema katika.uwanja wa ndege wa KIA
Godbless Lema akizungumza katika mkutano wa hadhara alioowasili nchini akitokea Canada aliokuwa akiishi uhamishoni.
**************************
Julieth Laizer ,Arusha
Arusha.Mwenyekiti wa Chadema Taifa amewataka wanachama wa chama hicho kuwa watulivu katika kipindi hiki cha maridhiano wakiwa wanapigania katiba mpya.
Mbowe ameyasema hayo leo machi 1,2023 katika mkutano wa hadhara wa kumpokea aliyekuwa aliyekuwa mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema uliofanyika katika viwanja vya reli jijini Arusha.
Hata hivyo Mwenyekiti huyo amesema ni wajibu wake kama kiongozi wa chama hicho kuhakikisha wanapigania upatikanaji wa katiba mpya itakayoleta maendeleo yenye haki kwa wananchi.
Hata hivyo Mbowe alimkabithi Lema kanda ya kaskazini kuhakikisha anaisimamia na kuwasisitiza kutokulala ikiwa sasa hivi Lema hana majukumu ya kifamilia kwani ameiacha nchini Canada.
Kwa upande wake ,Aliyekuwa Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema amesema wakati akitaka kurudi Tanzania alimpigia Rais Mstaafu Dk.Jakaya Kikwete ili aongee na Rais Samia Suluhu Hassan kuhusu kurudi kwake.
“Nilikimbia kwa sababu sikutaka kupuuza yale niliyoambiwa na hata nabii angenisikiliza asingeweza kufungwa(Mwenyekiti Mbowe)” amesema Lema.
Aidha Lema amesema kuwa,Lisu kabla ya kupigwa risasi siku moja kabla aliambiwa na Gwajima kuwa atapigwa risasi wakiwa East Afrika lakini hakusikiliza na alikwenda Dodoma ndipo alipopigwa risasi.
Amesema kuwa ,sasa hivi amerudi nchini kukipigania chama.chake ili wananchi waweze kupata haki ikiwemo upatikanaji wa chakula kutokana na gharama za maisha kuwa juu hivyo watatumia lugha za kistaarabu kiwasilisha hoja muhimu.
“Ushamba wa kukabana kabana ulikuwa ni undondosha na hata ukikaa kwenye jukwaa unatafuta maneno ya kumsema Rais unakosa kutokana na nidhamu yake lakini watatumia njia ya kumkaba kufikisha ujumbe bila lugha ya matusi.”amesema Lema .
Hata hivyo Lema amesema kuwa, ataanza kumshughulikia nabii ambaye anatoa sh.milioni 100 ikiwa nyumba yake ni nzuri kuliko kanisa la Mungu.