NAIBU Waziri Ofisi ya Rais ,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.Deogratius Ndejembi ,akizungumza wakati akifunga Kikao kazi cha Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa na Wakuu wa Idara za Utawala na Rasilimaliwatu katika Mamlaka za Serikali za Mitaa yaliyofungwa leo Februari 25,2023 jijini Dodoma.
SEHEMU ya Washiriki wakimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Rais ,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.Deogratius Ndejembi,wakati akifunga Kikao kazi cha Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa na Wakuu wa Idara za Utawala na Rasilimaliwatu katika Mamlaka za Serikali za Mitaa yaliyofungwa leo Februari 25,2023 jijini Dodoma.
KATIBU Mkuu, Ofisi ya Rais -Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,Dkt. Laurean Ndumbaro,akizungumza wakati wa Kikao kazi cha Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa na Wakuu wa Idara za Utawala na Rasilimaliwatu katika Mamlaka za Serikali za Mitaa yaliyofungwa leo Februari 25,2023 jijini Dodoma.
MKURUGENZI wa Idara ya Serikali za Mitaa, OR – TAMISEMI Bi. Angelista Kihaga,,akizungumza wakati wa Kikao kazi cha Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa na Wakuu wa Idara za Utawala na Rasilimaliwatu katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kilichofungwa leo Februari 25,2023 jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna-DODOMA
NAIBU Waziri Ofisi ya Rais ,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.Deogratius Ndejembi, amewataka watumishi kujenga tabia ya kusikiliza na kutolea ufafanuzi matatizo ya wananchi na wasisubiri mpaka taarifa ziwafikie viongozi wa juu.
Naibu Waziri Ndejembi ameyasema hayo leo Februari 25,2023,Jijini Dodoma ,wakati akifunga kikao kazi cha siku tatu cha Makatibu Tawala Wasaidizi na Wakuu wa Idara katika Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Amesema kuwa wanapaswa kukerwa sana na matatizo ya wananchi hususan wale wa Vijijini ambao wengi wao ni maskini wanaofika kutaka huduma kutoka kwa watumishi wanaowasimamia.
“Sio lazima viongozi wa juu ndio watolee ufafanuzi malalamiko ya wananchi wakati nyinyi mpo na mnawajibu wa kufanya hivyo kabla hayajafika mbali na imani yangu ni kwamba mtakwenda kuyatumia mafunzo haya katika kutatua changamoto za wananchi,” amesema Ndejembi
Aidha amesema kwa kuzingatia Utawala wa Sheria, Watumishi wa Umma na Wananchi katika maeneo yenu ya utawala wataweza kupata haki na stahiki zao kwa wakati bila kukwamishwa au kusumbuliwa wakati wa kupata huduma.
Hata hivyo Ndejembi amewaagiza watendaji hao kusimamia nidhamu ya watumishi kwa kuzingatia sheria za maadili ya utumishi wa umma na kutenda haki wakati wa kuwachukulia hatua za kinidhamu watumishi.
Amewasisitiza kuongoza kasi katika mapambano dhidi ya rushwa kwa kuziba mianya yote ya rushwa ,pamoja na kakusanya mapato ya serikali na kuwasimamia watumishi wenye dhamana ya kukusanya mapato wafanye kazi kwa uaminifu ili kufikia malengo ya serikali.
”Ni matumaini yangu kuwa kupitia Kamati za Kudhibiti Uadilifu zilizopo katika Halmashauri zenu suala hili mtalipa umuhimu na kuhakikisha kuwa mianya ya rushwa inadhibitiwa.”amesisitiza Ndejembi
Kwa upande wake Mkuu wa Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Halmashauri ya wilaya ya Rombo, Bi.Judith Mahende amesema kuwa wamepokea mafunzo na maelekezo yote waliyopatiwa katika kikao kazi hicho na watakwenda kuyafanyia kazi kwa ajili ya maslahi ya taifa na wananchikwa ujumla.
“Tumeyapokea mafunzo na maelekezo yote na tutakwenda kuyafanyia kazi katika halmashauri zetu,kwa mfano suala la nidhamu kwa watumishi wa umma,mapambano dhidi ya rushwa na ukusanyaji na usimamizi wa mapato ya serikali tutahakikisha yanatumika kama ilivyopangwa na kwa wakati,”amesema Mahende