MKUU wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa akizungumza wakati akifungua mafunzo kwa waandikishaji na waandaaji wa orodha ya wapiga kuwa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2019 ambapo aliwataka wawe makini ili wasijikute wameingia matatani kulia ni Afisa Tarafa ya Korogwe Michael John kushoto ni Msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Korogwe mji Kassim Kaoneka
Afisa Tarafa ya Korogwe Michael John akizungumza kwenye mafunzo hayo kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa
Mwanasheria wa Halamshauri ya Korogwe mji Mwanasheria wa Halmashauri ya Korogwe mji Madgalena John akizungumza wakati wa mafunzo hayo
Msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Korogwe mji Kassim Kaoneka akizungumza kulia ni Mkuu wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa
Sehemu ya waandikishaji na waandaaji wa orodha ya wapiga kura Korogwe wilayani Korogwe wakiwa kwenye mafunzo hayo
Sehemu ya waandikishaji na waandaaji wa orodha ya wapiga kura Korogwe wilayani Korogwe wakiwa kwenye mafunzo hayo
MKUU wa wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga Kissa Gwakisa amewaonya waandikishaji na waandaaji wa orodha ya wapiga kura wilayani humo watakaobainika kuwaingiza raia wa kigeni kwamba hawatasalimika badala yake watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.
DC Kissa aliyasema hayo leo wakati akifungua mafunzo kwa waandikishaji na waandaaji wa orodha ya wapiga kuwa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2019 ambapo aliwataka wawe makini ili wasijikute wameingia matatani.
Alisema kwamba pamoja na kuwepo kwa mafunzo hayo lakini wapo baadhi ya waandikishaji na waandaaji wa orodha ya wapiga kura kwenye uchaguzi huo wanaweza kufanya tofauti na maelekezo hivyo watahakikisha wanashughulikiwa kwa mujibu wa sheria zilizopo.
“Ndugu zangu wasimamizi uchaguzi wilayani, wanasimamia uchaguzi wasaidizi ngazi ya wilaya, Kata, Vijini na Mitaa kuhakikisha wanakuwa waaminifu na nidhamu wakati wa kutekeleza majukumu yenu na hii itasaidia kuepusha malalamiko huku akiwaonya watakaokwenda kunyume watachukuliwa hatua kali dhidi yao “Alisema DC Korogwe.
Aidha Mkuu huyo wa wilaya aliwataka wasimamizi hao kuwa mfano mzuri katika utekelezaji wa majukumu yao kwa kuhakikisha wanatenda haki ili uchaguzi uweze kwenda kwa haki na usalama bila kuwepo na malalamiko ya aina yoyote ile.
“Lakini pia niwaambie kwamba elimu hii muende kuitoa na ngazi za chini..kupiga kura ni haki ya kila mtanzania hivyo tunawategemea kama Taifa kundi hili lipo kila kila wilaya kwa nyie wa hapa nataka kuona mfano mzuri Korogwe Uchaguzi uende vizuri kusiwe na malalamiko”Alisema DC Kissa.
Hata hivyo alisema kwamba wataendelea kupewa semina ili kuweza kuwasaidia kuondokana na kufanya makosa kwenye uchaguzi huo ikiwemo kuzingatia nidhamu ya hali ya juu wakati mkitekeleza majukumu yenu mapya.
“Mpo kwenye nafasi nyeti Taifa linawategemea yale mambo siri mfanye siri lazima mtambua kwamba mnajukumu kubwa na zito kwa watanzania lakini mkizingatia maelekezio mnayopewa itakuwa chachu kubwa ya kusimamia vema uchaguzi bila kuwepo wa manunguniko”Alisema Mkuu huyo wa wilaya.
Awali akizungumza wakati akifungua mafunzo hayo Mwanasheria wa Halmashauri ya Korogwe mji Madgalena John alimuhaidi Mkuu huyo wa wilaya kwamba hawatamuangusha wala kuiangusha serikali na watakwenda kuitendea haki serikali yao na wananchi wa wilaya hiyo.
Alisema kwamba wanakwenda kufanya jukumu hilo nzito ambalo wamekabidhiwa na serikali na wanaimani baada ya neno kutoka kwake limewapa mwanga mpya ambao utakuwa chachu katika kutekeleza majukumu yao .
“Nikuhaidi Mh DC hatutakuangusha wewe wale serikali tutakwenda kuitendea haki serikali na wananchi wa korogwe jukumu hilo zito lakini tutalifanya kwa ufanisi mkubwa “Alisema .
Mwisho.