Na.Mwandishi Wetu-NJOMBE
Kaimu Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Njombe Noel Mseo mbele ya vyombo vya habari wakati akiwasilisha taarifa ya miezi mitatu ya utendaji kazi wao amesema miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa barabara,shule pamoja na vituo vya afya ambapo baada ya ukaguzi huo wamebaini kuwapo kwa kasoro hizo zikiwemo za kukiuka sheria za manunuzi.
Aidha Kamanda Mseo ameeleza kuwapo kwa mashine za kukusanyia mapato POS ambazo zimekuwa zikitumika kinyume cha sheria na baadhi ya maofisa wa serikali wanaokusanya ushuru.
Kituo hiki kimezungumza na wananchi mkoani Njombe juu ya vitendo vya ukiukwaji wa sheria unaofanywa na baadhi ya maofisa wa serikali ambapo baadhi yao akiwemo Menard Mlyuka mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Njombe na Fabian Mgeni mwenyekiti wa Jumuiya ya wafanyabiashara halmashauri ya mji wa Njombe wamesema hatua kali za kisehria zinapaswa kuchukuliwa kwa wanaokutwa kuhujumu miradi hiyo na kukiuka sheria za manunuzi.
Raia wengine akiwemo Wema Mbanga wamesema kukiukwa kwa sheria za manunuzi huenda kunatokana na aina ya upatikanaji wakandarasi kwani baadhi yao wamekuwa wakipata kazi kwa kufahamiana.
Ili kukabiliana na vitendo vya rushwa nchini Takukuru imelazimika kuanzisha programu ya Takukuru Rafiki inayojihusisha na utoaji elimu kupitia mikutano mbalimbali,vyombo vya habari pamoja na club za wapinga rushwa shuleni lengo likiwa ni kutaka kuzuia rushwa kabla haijatokea.