Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Ruvuma Jackilini Msongozi Ngonyani akizungumza na Viongozi wa UWT Wilayani Nyasa kabla ya kuwagawia majiko ya gesi
Mbunge Msongozi wa kwanza kushoto akikabidhi jiko la gesi kwa mmoja wa wanawake, wa kwanza kulia ni Katibu wa Mbunge Stambuli Nyale
Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Mbinga Grace Millinga(Mama Madereke) akifurahia kukabidhiwa jiko la gesi, wakwanza kushoto ni Mbbunge Msongozi
****************************
NA STEPHANO MANGO, MBINGA
JUMUIYA ya wanawake wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Ruvuma(UWT) wamempongeza Mbunge wa Vitimaalum Jacklini Msongozi Ngonyani kwa kuwajali na kuwagawia wanawake wa wilaya zote za mkoa wa Ruvuma majiko ya gesi 700 yenye thamani ya milioni 42
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wanawake hao walisema kuwa Mbunge Msongozi amekuwa jilani sana na Jumuiya ya UWT na kwa kuwawakilisha vyema wanawake na wananchi wa mkoa wa Ruvuma hasa katika kupigania maendeleo ya Mkoa,miongoni mwa mambo ambayo amekuwa akiyapigania ni pamoja masuala ya kilimo, elimu, afya na uwezeshwaji wanawake kiuchumi
Mwenyekiti wa Uwt Wilaya ya Songea Skola Ngonyani alisema kuwa Msongozi amekuwa mwakilishi mwenye kuguswa na hali za wanawake na wananchi wote Mkoani Ruvuma kwani amekuwa akijitahidi sana kutatua kero mbalimbali zinazowakabili
Ngonyani alisema kuwa majiko ya gesi ambayo wamepewa licha ya kwenda kuwarahisishia shughuli zao za mapishi majumbani lakini majiko haya yanakwenda kuwa nishati rafiki majumbani mwao na hivyo kuendelea kulilinda taifa letu na matumizi ya nishati zinazozuiliwa kama kuni na mkaa ambazo matumizi yake yana athari hasi kwa Taifa letu.
Naye Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Mbinga Grace Millinga(Mama Madereke) alisema kuwa anampongeza Mbunge Msongozi kwa juhudi zake za kuchochea maendeleo katika Mkoa huo ambapo pamoja na mambo mengine, ameunga mkono juhudi za wakulima kwa kuwagawia wanawake wa Mkoa huo jumla ya tani 7 za soya zenye thamani ya milioni 35
Millinga alisema kuwa Mbunge huyo amekuwa akichangia ujenzi wa Ofisi za Chama na Serikali, pia ujenzi wa zahanati na vituo vya afya kwa kutoa mabati na saruji pamoja na fedha taslim hali ambayo inaunga mkono jitihada za Rais Dkt Samia Suluhu Hassan za kuwaletea maendeleo watanzania
Akizungumza na wanawake hao kwa nyakati tofauti Mbunge wa Vitimaalum Mkoa wa Ruvuma Jacklini Msongozi Ngonyani alisema kuwa jukumu langu kubwa ni kuhakikisha kuwa ninawatumikia wanawake wa Mkoa wa Ruvuma kwa hali na Mali ili sikumoja na wao waweze kusimama kwa miguu yao.
Msongozi alisema kuwa yapo mazuri mengi yanakuja ambayo kwa pamoja tutakwenda kuyafurahia kama wana Ruvuma kikubwa tuendelee kumuomba Mungu atujaalie Afya Njema na Ufahamu ili tuweze kuyafaidi kwa pamoja.
Alisema kuwa kwakutambua umuhimu wa kuwarahisishia akinamama shughulizao ndio maana niliamua kuwagawia Majiko ya Gesi akinamama wa UWT Mkoa wa Ruvuma hawa wa wilaya ya Nyasa, pia nimegawa majiko hayo wilaya ya Songea, Namtumbo, Tunduru na Mbinga
Alieleza zaidi kuwa amegawa cherehani kwa wanawake wajasiliamali kutoka kwenye Wilaya zote za Mkoa wa Ruvuma 600 zenye thamani ya milioni 168, majiko ya gesi 700 yenye thamani ya milioni 42 na soya tani 7 zenye thamani ya shilingi milioni 35
Alisema kuwa panapo majaaliwa tutasimama na kufanya kazi pamoja kwenye nyanja zote kuanzia Afya, Elimu, Ujasiliamali, Kilimo na mengineyo lengo likiwa ni kuhakikisha tunamkomboa Mwanamke wa Mkoa wa Ruvuma.