***************************
NJOMBE
Makahakama ya hakimu mkazi Njombe imeanza kusikiliza kesi no 2 ya mwaka 2022 ya madai ya fidia iliyofunguliwa na msimamzi wa mirathi wa marehemu kasirida mlowe dhidi ya kanisa la KKKT Dayosisi ya kusini .
Kesi hiyo ya madai ambayo imeanza kusikilizwa kwa upande wa mashahidi wa mlaklamikaji ilifunguliwa baada ya msimamizi wa mirathi kushinda trafic kesi no 6 , 2021 iliyotokea eneo la Kibena mlima wa Ichunilo septemba 25, 2020 ikihusisha gari aina hiace yenye no za usajili T298 DNE na gari yenye no T210-AHU Mercedes Benzi Track mali ya kanisa la KKKT Dayosisi ya kusini na kupelekea majeraha mabaya ya kichwa na kuvunjika mguu na kisha kupoteza uhai akiwa hospitali.
Akitoa ushahidi mahakamani shahidi namba moja wa upande wa mlalamikaji Bi Sigrada Mligo,baada ya kutoa vielezo vitakavyosaidia kutoa hukumu ya kesi hiyo amesema wamelazimika kufungua kesi ya madai baada ya mahakama ya wilaya ya Njombe kutoa hukumu ya kesi ya ajali ya barabarani iliyomkuta na hatia dereva wa gari la kkkt ya kuendesha gari lisilo na breki,lisilo na bima na makosa mengine likiwemo la kuendesha gari bila kuwa na mkataba.
Baada kuwasilisha vielelezo 8 vitakavyotumika kwenye kesi na kimoja ambacho ni ripoti ya daktari kukataliwa kwasababu kilikuwa ni kopi ,shahidi akaiomba mahakama kumpa muda kuleta ripoti halisi ya daktari na kisha kutoa ombi la msingi kwa mahakama kutoa Oder kwa kkkt ya kulipwa fidia ya mil 100 na ghara za kesi kwa kitendo cha gari lake kukatisha maisha ya mtu ambaye alikuwa mjasiriamali mdogo ,mwenye kundi kubwa la watu wanaomtegemea nyuma wakiwemo watoto wake watatu na wazazi wake ambao ni wazee sasa.
Katika hatua nyingine bi Mligo amesema ni jambo la heri marehemu enzi za uhai wakati akipigania uhai hospitalini alitembelewa na katibu mkuu wa dayosisi na kisha kutoa pole ya sh.100,000 lakini punde baada ya mgonjwa kufariki dunia ,shida ikawa kwa wategemezi wake ambao ni watoto waliotawanywa kwa ndugu .
Kesi hiyo iliyoendeshwa na hakimu wa mahakama ya hakimu mkazi Njombe Liad Chamshama ambayo kwenye upande wa mlalamikaji imewakilishwa na mawakili watatu akiwemo Emmanuel Chengula ,Frank Ngafumika na Gerevas Semgabo huku upande wa mlalamikiwa ukiwakilishwa na wakili msomi Marco Kisakali imeahirishwa hadi hapo marchi 10 ushahidi utakapoendelea kusikilizwa.