Na Mwandishi wetu
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma imeendelea na zoezi la kutangaza mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita kwa taasisi zilizopo Mkoani, Mhe. Rosemary Senyamule amesema mafanikio yaliyopo kwenye Mamlaka ya Mapato ya Dodoma, kumekuwa na ongezeko la fedha kutoka kwenye Halmashauri na kuwezesha maendeleo ndani ya Mkoa wa Dodoma.
Amesema Mkoa wa Dodoma ulipangiwa fedha za maendeleo kiasi cha Shillingi billioni 32.1 kwenye miradi ya maendeleo mwaka 2021 na mwaka 2022-2023 kiasi cha billioni 35.1 ni sawa na ongezeko la asilimia 9 fedha ongezeko la mapato ya ndani za Halimashauri zimewezesha ujenzi wa vituo vya Afya 4,Zahanati 12 na Madarasa 135.
Senyamule amesema,kuongezeka kwa mapato ya Halmashauri za mkaoa itafanya wananchi wataendelea kuongezewa mikopo utawawezesha kuanzisha biashara na kukuza biashara na uwezo wa kiuchumi ambalo ndio lengo la serikali kuwatengenezea wananchi mazingira mazuri.
“Mkoa wa Dodoma ulipangiwa fedha za maendeleo kiasi cha Shillingi billioni 32.1 kwenye miradi ya maendeleo mwaka 2021 na mwaka 2022-2023 kiasi cha billioni 35.1 ni sawa na ongezeko la asilimia 9 fedha zimeongezeka kama mapato ya ndani ya Halimashauri zimewezesha ujenzi wa vituo vya Afya 4,Zahanati 12 na Madarasa 135.
“kama tunavyojua kuongezeka kwa mapato ya Halmashauri za mkaoa itafanya wananchi wataendelea kuongezewa mikopo utawawezesha kuanzisha biashara na kukuza biashara na uwezo wa kiuchumi ambalo ndio lengo la serikali kuwatengenezea wananchi mazingira mazuri,”amesema.
Meneja Msaidizi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania mkoa wa Dodoma, Sylver Rutagwelera ameelezea mafaniko yaliopatika kwenye taasisi hiyo katika kipindi cha miaka miwili.
Amesema katika kuhaikikisha Mamlaka ya Mapato inapanua wigo wa walipakodi na kuongeza makusanyo ya kodi,Mamlaka ya Mapato Mkoa wa Dodoma imefanikiwa kusajili walipakodi wapya 12,076 kwa kipindi cha kuanzai Januari 2021 hadi Disemba 2022 hii imetokana kuepo na serikali ya awamu ya sita kuimarisha mahusiano mazuri kati yake ma walipakodi.
Lakini pia,Mamlaka ya Mapato Mkoa wa Dodoma imefanikiwa kusajili walipa kodi wapya 2,237 wanaotumia Mashine za kieletroniki kwa mwaka 2022 pekee sambamba na hilo mkoa umeendelea kusimamia matumizi ya mashine za EFD kwa kutoa elimu na pia kutoa adhabu kwa wanaokiuka sheria.
“katika kuhaikikisha Mamlaka ya Mapato inapanua wigo wa walipakodi na kuongeza makusanyo ya kodi,Mamlaka ya Mapato Mkoa wa Dodoma tumefanikiwa kusajili walipakodi wapya 12,076 kwa kipindi cha kuanzai Januari 2021 hadi Disemba 2022 hii imetokana kuepo na serikali ya awamu ya sita kuimarisha mahusiano mazuri kati yake ma walipakodi.
Hata hivyo,Mamlaka imefanikiwa kutoa elimu kwa walipa kodi na jamii kwa ujumla ili kodi ilipwe bila shuruti na matumizi ya nguvu yasio na lazima pia imekuwa ikisimamia na kudhibiti makusanyo ya kodi.
Rutagwelera ameeleza katika kuhakikisha wanaongeza makusanyo ya kodi mamlaka ya mapato Mkoa wa Dodoma imejipanga kutekeleza ufatiliaji wa karibu wa matumizi ya mashine za EFD na ufatiliaji na usajili wa wafanyabishara wapya kwenye kodi ya mapato ma kodi ya ongezeko la thamani.
Hata hivyo, ameelezea changamoto katika ukusanyaji wa mapatao licha ya kutoa elimu ya kutosha imekuwa bado wafanyabiashara na wanachi wamekuwa hawana elimu ya kutosha na ndio maana wamekuwa wakitoa elimu hasa pembezoni mwa mji katika vijiji Chipogolo,Mtera,Mbande,Songambele,Tubugwe,Hombolo,Mvumi misheni,Kibakwe na Wilaya Bahi,Chemba,Chamwino, na Kondoa.