WANAWAKE ambao wanatatizo la kupata watoto wameshauriwa kutumia njia ya kisasa ya kupandikiza mimba ili waweze kuondokana na tatizo hilo.
Rai hiyo imetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Mratibu wa Chennai Ferlity Centre and Research Institute(CFC)Shose Kombe,wakati wa maonesho maonesho ya afya yanaofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubili yalioanza tarehe 16 february mwaka mpaka tarehe 18 february mwaka huu.
Kombe amesema wamama wanaotafuta watoto wanatakiwa kujitokeza kwenye maonesho hayo ambapo kuna madaktari bingwa kutoka CFC ambao wanawamekuja kuja kushiriki maonesho hayo nakuweza kutatua changamoto ya ugumba kwa wakina wanawake.,
Aidha,Kombe amesema madakari hao watakuwepo siku zote ambapo watatoa hudumu hiyo bure na kuwataka wanawake waliokata tamaa wajitokeze kupata huduma ya upandikizaji.
Kwa upande wake Daktari Bingwa kutoka CFC,Dr Thomas vidingadu,amesema kwa sasa wamedhamilia kumsaidia mwanamke wa kiafrika anayetaka kupata mtoto kwa kuweka bei nafuu .
Hata hivyo,Dkt Vidingadu amesema kwa sasa wapo Tanzania wanatazamia kuenea sehemu mbalimbali Afrika na kusema huduma wanayoitoa haina matatizo yoyote kwa binadamu na kuwataka kujitokeza kupatiwa huduma.