KATIBU Msaidizi -Kanda ya Kati,Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Bi.Jasmin Awadhi Bakari,akizungumza wakati wa mafunzo kwa Madiwani,Wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri ya Chemba yaliyoandaliwa na Ofisi ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma leo Februari 16,2023 wilayani Chemba Mkoani Dodoma.
MWENYEKITI wa Halmashauri ya Chemba, Sambala Said,akizungumza wakati akifungua mafunzo kwa Madiwani,Wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri ya Chemba yaliyoandaliwa na Ofisi ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma leo Februari 16,2023 wilayani Chemba Mkoani Dodoma.
KATIBU Msaidizi -Kanda ya Kati,Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Bi.Jasmin Awadhi Bakari,akizungumza wakati wa mafunzo kwa Madiwani,Wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri ya Chemba yaliyoandaliwa na Ofisi ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma leo Februari 16,2023 wilayani Chemba Mkoani Dodoma.
SEHEMU ya Washiriki wakifatilia mada mbalimbali wakati wa mafunzo kwa Madiwani,Wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri ya Chemba yaliyoandaliwa na Ofisi ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma leo Februari 16,2023 wilayani Chemba Mkoani Dodoma.
AFISA kutoka Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Modesta Mtui,akitoa mada kwa Madiwani,Wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri ya Chemba wakati wa mafunzo yaliyoandaliwa na Ofisi ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma leo Februari 16,2023 wilayani Chemba Mkoani Dodoma.
Na.Alex Sonna-CHEMBA
MADIWANI na wataalamu katika Halmashauri ya Chemba wametakiwa kuacha migogoro na badala yake washirikiane katika uendaji kazi wao ili kuwaletea maendeleo wakazi wa Halmshauri hiyo.
Hayo yameelezwa leo Februari 16,2023 wilayani Chemba na Katibu Msaidizi -Kanda ya Kati,Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Bi.Jasmin Awadhi Bakari, wakati akifungua mafunzo kwa Madiwani na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri hiyo yaliyoandaliwa na Ofisi ya Sekretarieti ya Maadili ya viongozi wa Umma.
Bi.Jasmin amesema kuwa katika siku za hivi karibuni kumekuwa na mvutano kati ya madiwani na wataalamu katika Halmashauri mbalimbali.
“Tukaona ili tuweze kuisaidia serikali tuwakumbushe wanatakiwa kufanya nini tunawasisitiza kufanya kazi kwa pamoja wajue yanaeleweka lengo lao ni nini dira yao ni nini
“Wanatakiwa kufanya kazi kwa pamoja ili watende kwa kuwatimizia mahitaji wananchi,wakiwa hawana maeleano itakuwa ngumu ndio maana tukaona tufanye mafunzo haya,”amesema Jasmin.
Aidha amesema mafunzo kama hayo wameyafanya pia mkoani Singida katika wilayani za Itigi na Kalambo na wanaendelea na wilaya zingine.
“Tumekuja kutoa mafunzo Halmashauri Chemba ikiwa ni moja kati ya Halmashauri 15 tunazozisimamia katika Halmashauri ya Chemba lengo kubwa ni kukumbushana na kuwakumbusha viongozi na watumishi katika uwajibikaji wa pamoja.
“Tunawajibu wa kuwasimamia na wanafanya kazi kwa kushirikiana kwa pamoja ili kufikia malengo kubwa ni kuwapatia maendeleo,”amesema
Kuhusu mmomonyoko wa maadili kwa viongozi wa kanda ya kati Kamesema kuwa amesema sio mkubwa na wamekuwa wakiwakumbusha umuhimu wa kufuata maadili katika utendaji kazi wao wa kila siku.
“Binadamu ameumbwa kukumbushwa na ni mtu wa kujisahau sasa ili kuisaidia serikali ndio maana tunatoa mafunzo ya mara kwa mara ili fedha zisiende mahakamani ziende kwenye miradi ya wananchi,”amesema Jasmin.
Kwa upande wake,Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chemba, Sambala Said, amesema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo katika utendaji kazi wao.
Amesema kiongozi ni lazima afuate maadili ya utendaji kazi kwani yeye anamilikiwa na umma hivyo ni lazima ahakikishe anavaa vizuri pamoja na matendo yake yanakuwa mazuri.
“Ndio maana kila mwaka anatakiwa atoe tamko la kukiri mali anazomiliki yeye na familia yake ili kumfanya kiongozi kuwa kioo cha jamii.
“Kuna baadhi wanakosa maadili na tumekuwa tukishuhudia kiongozi wa umma kutaka jambo lake, mfano kuomba rushwa ya fedha na ngono,”amesema Bw.Said
Amesema mafunzo hayo ni muhimu na yanatengeneza ramani ya kujua viongozi wa uuma anatakiwa aishi vipi na jamii inayomzunguka.
Hata hivyo ametoa wito kwa viongozi wa umma kuhakikisha wanafuata wajibu wao pamoja na kuyafanyia kazi mafunzo wanayofundishwa.