MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango,akizungumza
wakati wa hafla ya kukabidhi magari 54 kwa kwa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) pamoja na Pikipiki 916 kwa Watendaji Kata zilizotolewa na Ofisi ya Rais – TAMISEMI, hafla iliyofanyika leo Februari 14,2023 jijini Dodoma.
SEHEMU ya Viongozi Wakisikiliza hotuba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango,(hayupo pichani) wakati wa hafla ya kukabidhi magari 54 kwa kwa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) pamoja na Pikipiki 916 kwa Watendaji Kata zilizotolewa na Ofisi ya Rais – TAMISEMI, hafla iliyofanyika leo Februari 14,2023 jijini Dodoma.
WAZIRI wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Angellah Kairuki,akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi magari 54 kwa kwa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) pamoja na Pikipiki 916 kwa Watendaji Kata zilizotolewa na Ofisi ya Rais – TAMISEMI, hafla iliyofanyika leo Februari 14,2023 jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Jenista Mhagama,
akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi magari 54 kwa kwa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) pamoja na Pikipiki 916 kwa Watendaji Kata zilizotolewa na Ofisi ya Rais – TAMISEMI, hafla iliyofanyika leo Februari 14,2023 jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bw.Daniel Chongolo ,akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi magari 54 kwa kwa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) pamoja na Pikipiki 916 kwa Watendaji Kata zilizotolewa na Ofisi ya Rais – TAMISEMI, hafla iliyofanyika leo Februari 14,2023 jijini Dodoma.
KATIBU Mkuu wa Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Prof.Riziki Shemdoe, akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi magari 54 kwa kwa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) pamoja na Pikipiki 916 kwa Watendaji Kata zilizotolewa na Ofisi ya Rais – TAMISEMI, hafla iliyofanyika leo Februari 14,2023 jijini Dodoma.
MKUU wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule,akitoa salamu za Mkoa wakati wa hafla ya kukabidhi magari 54 kwa kwa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) pamoja na Pikipiki 916 kwa Watendaji Kata zilizotolewa na Ofisi ya Rais – TAMISEMI, hafla iliyofanyika leo Februari 14,2023 jijini Dodoma.
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akikata utepe kuashiria kukabidhi rasmi magari 54 kwa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) pamoja na Pikipiki 916 kwa Watendaji Kata zilizotolewa na Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Hafla iliofanyika leo tarehe 14 Februari 2023 jijini Dodoma . (Kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – TAMISEMI Angellah Kairuki na Mkuu wa Mkoa Manyara Makongoro Nyerere, Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Jenista Mhagama, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Daniel Chongolo na Mkuu wa Mkoa Dodoma Rosemary Senyamule)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akiwa na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Daniel Chongolo wakati akijaribu moja kati ya magari 54 yaliokabidhiwa kwa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) katika hafla iliyofanyika leo Februari 14,2023 jijini Dodoma.
MUONEKANO wa Magari pamoja na Pikipiki zilizokabidhiwa kwa Mameneja wa Mikoa na Wilaya wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini(TARURA) na Watendaji wa kata.
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akimkabidhi Afisa Mtendaji Kata ya Ng’ong’ona (Kulia) iliopo Dodoma moja kati ya Pikipiki 916 zilizotolewa kwa Watendaji Kata kutoka Ofisi ya Rais – TAMISEMI, katika hafla iliYofanyika leo tarehe 14 Februari 2023 jijini Dodoma.
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na Baadhi ya Watendaji Kata kutoka maeneo mbalimbali ya nchi wakati wa hafla ya kukabidhi Magari 54 kwa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) pamoja na Pikipiki 916 kwa Watendaji Kata zilizotolewa na Ofisi ya Rais – TAMISEMI,hafla iliyofanyika leo Februari 14,2023 jijini Dodoma.
Na Alex Sonna-DODOMA
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango amewataka watendaji wa kata nchini kuhakikisha wanasimamia haki na wanajiepusha kuonea wananchi.
Dk.Mpango ametoa kauli hiyo wakati wa hafla ya kukabidhi magari 54 kwa kwa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) pamoja na Pikipiki 916 kwa Watendaji Kata zilizotolewa na Ofisi ya Rais – TAMISEMI, hafla iliyofanyika leo Februari 14,2023 jijini Dodoma.
jijini Dodoma wakati wa hafla ya kukabidhi magari kwa Mameneja wa Mikoa na Wilaya wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini(TARURA) na Pikipiki kwa watendaji wa kata.
Dkt. Mpango amesema kuwa Serikali Kuu imekuwa ikipokea tuhuma nyingi za ukiukwaji wa maadili ya viongozi wa umma zinazofanywa na baadhi ya maafisa watendaji wa kata.
“Msijifanye miungu watu kwa kuwakamata wananchi na kupora mali zao kwa uonevu bila sababu za msingi, simamieni sheria lakini msionee watu, narudia simamieni sheria msionee watu,” amesema Dkt. Mpango
Hata hivyo amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri nchini kufuatilia tuhuma hizo na kuchukua hatua stahiki za kisheria na kinidhamu.
Aidha Dk.Mpango amesema kuwa watendaji wa kata ni viongozi muhimu katika utekelezaji wa shughuli za Serikali hivyo vyombo vya usafiri walivyokabidhiwa vitaongeza ufanisi wa kazi za Serikali endapo vitatumika kama ilivyokusudiwa.
“Nataka pikipiki hizi tunazogawa leo zitumike kuwafikia wananchi kwa urahisi, kuwasilikiza kuwahudumia na si kwa manufaa yenu binafsi”amesisitiza Dk.Mpango
Makamu wa Rais ameutaka Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) kufanya kazi kwa weledi na uaminifu ili kuyatimiza vema majukumu yao hususani ya kusimamia shughuli za ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya barabara.
Kwa upande wake Waziri wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Angellah Kairuki, amesema Rais alikubali pendekezo la kutumika Sh.Bilioni 2.9 za mgao wa kodi ya majengo za kuanzia Julai 2021 hadi Februari 2022 ili kununua vitendea kazi hivyo kwa watendaji wa kata.
”Lengo la vitendea kazi hivyo ni kuongeza ufanisi katika utoaji huduma kwa wananchi, kurahisisha usafiri pamoja na kuimarisha mapato.”amesema Waziri Kairuki
Aidha Waziri Kairuki amesema kuwa TAMISEMI inapanga kutumia biashara ya kaboni kama hatua ya kulinda mazingira pamoja na kuongeza vyanzo vya mapato kwa wananchi na Halmashauri kwa ujumla.
Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Jenista Mhagama amesema Serikali inatarajia kuongeza wahandisi pamoja na wakadiriaji majengo katika halmashauri ili kukabiliana na tatizo la ujenzi wa miundombinu chini ya kiwango.
Awali Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bw.Daniel Chongolo ametoa wito kwa serikali kufanya mapitio ili kutambua upande wenye tija katika ukusanyaji mapato hususani kodi ya majengo kati ya Serikali kuu na Tamisemi ili kupewa jukumu la ukusanyaji na kupata matokeo makubwa zaidi.
” Ameiomba serikali kuendelea kuongeza bajeti ya TARURA ili iweze kufungua zaidi miundombinu maeneo mengi zaidi yenye fursa na uzalishaji hapa nchini.”amesema Chongolo