Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
WAHAMIAJI haramu wawili raia wa Nigeria na Cameroon wamekamatwa Mapinga Kibosha, Mkoani Pwani kwa kosa la kuishi nchini kinyume cha sheria pamoja na utakatishaji fedha bandia na hati za kusafiria ,hali ambayo ingeweza kusababisha athari kiuchumi.
Kufuatilia hali hiyo Mwenyekiti wa kamati ya usalama, mkoa wa Pwani alhaj Abubakari Kunenge , alieleza hatomvumilia raia yeyote wa nje atakaetaka kuishi Mkoani humo kinyume na Utaratibu ambapo ameeleza wale wanaoishi bila kufuata sheria na kubainika watachukuliwa hatua.
Alieleza ,Mcameroon Bertrand Noubissie alikutwa na karatasi zilizoandaliwa kwa kwa ajili kuchapisha noti bandia za pesa,kemikali na kasiki la kutunzia fedha.
Wakati wa upekuzi mtuhumiwa Livingston Ese Onayomake raia wa Nigeria alikutwa na Jumla ya pasipoti 34 ambazo si za kwake, ambapo kati ya hizo pasipoti 32 ni za Nigeria na pasipoti mbili ni za Ghana .
“Alipohojiwa alidai kuwa alichukua pasipoti hizo kwa lengo la kuwatafutia viza ya Uturuki wahusika”
Kunenge alieleza kwamba ,mkoa huo sio eneo salama la uhalifu Wala kuingia kiholela,na vyombo vyote vya kiusalama vimejipanga.
Nae ofisa uhamiaji mkoa wa Pwani,Omary Hassan alieleza “Tarehe 9 mwezi huu tulipokea taarifa fiche kutoka kwa msiri wetu kwamba katika eneo la Mapinga,Kibosha kuna watu ambao uraia na mienendo yao inatia mashaka,,Tarehe 10 timu ya Maafisa Uhamiaji walifanikiwa kufika katika eneo husika na kutekeleza jukumu lao ambapo walikamata raia wawili wa Afrika Magharibi kutoka Mataifa ya Cameroon na Nigeria Sambamba na kuwafanyia upekuzi maungoni na kwenye makazi yao”
“Raia hawa wa kigeni walikuwa wakiishi nyumbani kwa bi.New Era Nyirembe mwanamke kabila Mjita ambae kwasasa ni marehemu na alikuwa mke wa mtuhumiwa Bertrand Noubissie raia wa Cameroon “alieleza Hassan.
Hassan alikiri matukio ya aina hiyo kutokea na sio mara ya kwanza.