MTENDAJI Mkuu wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) Dkt.Matiko Mturi,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Baraza hilo leo Februari 13,2023 jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna-DODOMA
Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) limesema limejipanga kukamilisha muongozo wa gharama za ujenzi wa barabara nchini kwa kuaandaa gharama za msingi za mkandarasi katika kutekeleza kazi mbalimbali za ujenzi wa barabara kwa kila mkoa Tanzania bara
Hayo yamesemwa leo Februari 13,2023 jijini Dodoma na Mtendaji Mkuu wa Baraza la Taifa la Ujenzi Dkt.Matiko Mturi,wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Baraza hilo.
Dk.Mturi amesema kuwa wameandaa mapendekezo ya kuboresha sheria na miongozo inayosimamia ujenzi wa majengo nchini.
‘’Tumeandaa viwango msawazo vya majengo ya Serikali,kutoa mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau wa Sekta ya ujenzi pamoja na kutoa ushauri wa kiufundi kwa wadau mbalimbali wa sekta ya ujenzi’’amesema Dkt.Mturi
Aidha amesema kuwa wameandaa kutoa fahirisi za bei za vifaa,mitambo na ujira katika shughuli za ujenzi kwa kila mwezi ili kuonesha mabadiliko ya bei ya vifaa vya ujenzi.
Pia kusimamia utatuzi wa migogoro inayotokea katika miradi ya ujenzi,kuandaa maandalizi ya kuwa na wiki ya ujenzi nchini na kukamilisha maandalizi ya kanuni za utekelezaji wa sheria ya baraza hilo.
Hata hivyo ameeleza kuwa wanaendelea kutoa ushauri wa kitaaluma kwa wadau wa sekta ya ujenzi na kuanza maandalizi ya awali ya wiki ya ujenzi nchini inayotegemewa kufanyika mwezi Septemba mwishoni na Oktoba.
Vile vile ameongeza kuwa wanaendelea kuratibu utatuzi wa migogoro inayotokea katika miradi ya ujenzi .
Dkt. Mturi amesema kuwa wanataka kuanzisha kituo cha Taarfia za Sekta ya Ujenzi ambacho kitakuwa muhimu sana kwa wadau kupata taarifa muhimu za sekta hiyo ikiwa ni pamoja na kuendeleza tafiti, teknolojia na ubunifu.
Ikumbukwe Baraza la Taifa la Ujenzi ni taasisi ya Serikaliiliyoanzishwa kwa sheria ya Bunge namba 20 ya mwaka 1979 na kufanyiwa marekebisho mwaka 2008 kwa lengo la kusimamia maendeleo ya sekta ya ujenzi ,