MTENDAJI Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Justina Mashiba,akizungumza na waandishi wa habari leo Februari 13,2023 Jijini Dodoma, kuhusu utekelezaji wa shughuli mbalimbali za mfuko huo.
Na.Alex Sonna-DODOMA
MTENDAJI Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Justina Mashiba amesema kuwa jumla ya shule 811 nchini zimefikishiwa Vifaa vya TEHAMA ambapo kwa wastani kila shule imepewa Kompyuta 5, Printa 1 na Projekta 1.
Hayo ameyabainisha leo Februari 13,2023 Jijini Dodoma,wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa shughuli mbalimbali za mfuko huo.
Bi.Mashiba amesema kuwa katika mradi wa kupeleka vifaa vya TEHAMA hadi sasa shule hizo zimefikiwa.
“Kwa mwaka wa fedha 2022/23, Shule 150 zitafikishiwa vifaa vya TEHAMA Bajeti kwa mwaka wa fedha 2022/23 ni Sh.1,950,000,000,”amesema Bi.Mashiba
Aidha Mashiba amesema kuwa Mradi wa kupeleka vifaa maalum vya kujifunzia kwa shule zenye watoto wenye mahitaji maalum
Shule 16 zimefikishiwa vifaa vya TEHAMA ambavyo ni pamoja na TV, Braille Machine (Nukta Nundu) Orbit reader (Machine za Kisasa), Laptops, Embosser (Printa ya nukta nundu).
Amesema shule zitakazonufaika ni pamoja na shule ya Sekondari ya Mpwapwa (Mpwapwa-Dodoma), Sekondari ya Mkolani (Mwanza), Sekondari ya Kashaulili (Mpanda-Katavi), Sekondari ya Morogoro (Morogoro).
Shule nyingine ni Sekondari ya Shinyanga (Kishapu-Shinyanga), Sekondari ya Wavulana Songea (Songea), Sekondari ya Kazima (Tabora) na Sekondari ya Haile Selassie (Mjini Magharibi) ambapo gharama zikazotumika ni Sh. 575,000,000.
Hata hivyo Mashiba amesema kuwa Mwaka 2009 Population Coverage ya Huduma za Simu ilikuwa asilimia 45 (45%) wakati kwa sasa imeongezeka hadi kufikia asilimia 96 (96%),Teknolojia ya 2G coverage yake ni 96%,3G ni 72%,4G ni 55% na Geographical Coverage ya 2G ni 69%; 3G ni 55% na 4G ni 36%.
Kwa upande wa Ujenzi wa Minara Vijijini amesema UCSAF imeingia mikataba kufikisha huduma katika kata 1,242 zenye vijiji 3,654, Wakazi 15,130,250 ambapo Minara 1,087 yenye vijiji 3,378 na wakazi 13,320,750 na Utekelezaji unaendelea katika Minara 155 yenye vijiji 276 na wakazi 1,809,500 kwa ruzuku iliyotolewa yaTZS bilioni 199 ikiwemo pia Mradi wa kimkakati wa Zanzibar, Minara 42, Shehia 38 ruzuku TZS bilioni 6.9.