Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha
Chama Cha Mapinduzi( CCM )Kibaha Vijijini, Mkoani Pwani, kimeanza mkakati maalum wa kuhamasisha wanachama wapya kujiunga na CCM wilayani humo,ambapo hadi sasa kimefikisha Jumla ya wanachama 39,100.
Akizindua rasmi mpango huo ,Viwanja vya Mtongani, Mwenyekiti wa CCM Kibaha Vijijini Mkali Kanusu alieleza ,kila Chama Cha siasa kinalilia uhai wa Chama chake kwa kuongeza mtaji wa wanachama.
Alieleza, kazi kubwa waliyonayo kwa Sasa kuanzia vijiji, vitongoji,kata na wilaya ni kuhamasisha wanachama wapya kujiunga na CCM ,kwani sababu zipo za ushawishi ikiwemo utekelezaji mkubwa wa ilani unaofanywa na Serikali iliyopo madarakani.
Kanusu alitoa Rai kwa makatibu,wenyeviti,wenezi wa ngazi zote kuingia kazini ili kuongeza mtaji wa Chama.
“Chama chetu Sasa kina wanachama 39,100 ,kazi hii sio ya leo tuu ,ilianza na tunaendelea kuifanya ,tunakwenda na mkakati maalum wa kusajili wanachama wapya,kulipa ada ,kujisajili katika mfumo “
“Dhamira yetu kila siku asubuhi tutasajili wanachama wapya ,nimezindua Leo Tutahakikisha kila siku tunaongeza wanachama wapya, kazi yetu kubwa Chama kiendelee kushuka Dola ,Wanachama ndio mtaji wetu, kulipa ada, kujiunga na Chama,”hii ndio kazi yetu,”alisisitiza Kanusu.
Kanusu alifafanua ,chama chetu bado kinaheshimika na kinaendelea kushika Dola ,hivyo ni Lazima kuendelea kumpa moyo Mwenyekiti wa CCM Taifa dkt. Samia Suluhu Hassan na kumuunga mkono kwa jitihada na kazi kubwa anayoifanya ndani ya nchi kusimamia utekelezaji wa ilani na miradi ya kimkakati,ya kati na midogo ikitekelezwa katika nyanja zote.
Katibu wa CCM Kibaha Vijijini Safina Nchimbi alieleza , wanaendelea kusimamia utekelezaji wa ilani,kutembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali katika nyanja zote ili kujiridhisha na utekelezaji wake.