Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma za Sheria Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Dustan Shimbo leo Februari 11, 2023 akiwasilisha mada kuhusu Sheria ya Usimamizi wa Mazingira (Kanuni za Kudhibiti Kemikali Zinazoharibu Tabaka la Ozoni), 2022, katika siku ya pili mafunzo kwa maafisa wa Serikali waliopo katika mpaka wa Horohoro mkoani Tanga, kuhusu udhibiti wa uingizaji nchini wa gesi na vifaa vyenye gesi zinazomong’onyoa tabaka la ozoni.
Maafisa wa Serikali waliopo mpaka wa Horohoro mkoani Tanga wakifuatilia mafunzo kwa maafisa wa Serikali waliopo katika mpaka wa Horohoro mkoani Tanga, kuhusu udhibiti wa uingizaji nchini wa gesi na vifaa vyenye gesi zinazomong’onyoa tabaka la ozone yaliyoanza jana Februari 10, 2023 na kuhitimishwa leo Februari 11, 2023.
Mhandisi Goodluck Lulagora kutoka Wakala wa Mafunzo ya Elimu ya Uvuvi Bagamoyo (FETA) akitoa mafunzo kwa maafisa wa Serikali walipoko mpaka wa Horohoro mkoani Tanga kuhusu Matumizi ya Mitambo ya Kutambua Gesi zinazoharibu Tabaka la Ozoni yaliyoanza jana Februari 10, 2023 na kuhitimishwa leo Februari 11, 2023.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mazingira, Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Catherine Bamwenzaki akiwa katika picha ya pamoja na maafisa wa Serikali waliopo katika mpaka wa Horohoro mkoani Tanga wakati wa mafunzo kuhusu udhibiti wa uingizaji nchini wa gesi na vifaa vyenye gesi zinazomong’onyoa tabaka la ozoni yaliyoanza Februari 10, 2023 na kuhitimishwa leo Februari 11, 2023.