WAZIRI wa Maliasili na Utalii,Balozi Dkt.Pindi Chana akizungumza na wananchi wa Kata ya Mninga kufuatia ombi lao kumegewa sehemu ya eneo la Hifadhi kwa ajili ya ujenzi wa zahanati kukubaliwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan umetokana na yeye Rais kuguswa na kujali afya na maendeleo ya maisha ya wananchi wake.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dkt.Pindi Chana akikata utepe katika eneo la Hifadhi la Shamba la Miti.Sao Hili ambapo Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameridhia eneo hilo lenye ukubwa wa ekari 10 limegwe ili Zahanati ya Kata ya Mninga ijengwe
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mufindi ambaye ni Diwani wa Kata ya Mninga, Mhe.Festo Mgina akizungumza na wananchi wa Mninga amvapo amesema anamshukuru sana Rais Samia Hassan kwa kukubali ombi la wananchi wa Mninga kumegewa eneo la Hiifadhi kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali
Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dkt.Pindi Chana ( katikati ) akielekea kukagua eneo la ekari 10 ambalo ni sehemu ya shamba la miti la Miti Sao Hili ambalo Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameridhia eneo hilo limegwe ili Zahanati ya Kata ya Mninga iweze kujengwa, Wengine aliombatana nao ni baadhi ya madiwani ww Halmashauri ya wilaya ya Mufindi.
………………………………….
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan ameridhia ombi la kumegwa eneo la ekari 100 lililokuwa linamilikiwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ( TFS ) kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati ya Kata ya Mninga iliyopo wilayani Mufindi mkoani Iringa
Akizungumza na wananchi wa Kata ya Mninga wilayani Mufindi, Iringa Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dkt.Pindi Chana ameeleza kuwa uamuzi huo wa Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan umetokana na yeye kuguswa na kujali afya na maendeleo ya maisha ya wananchi wake.
Amesema eneo hilo lililomegwa ni moja ya sehemu ya Shamba la Miti la Sao Hill ambalo lina miti ya kupandwa aina ya misindano yenye zaidi ya miaka mitano lakini hata hivyo Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amekubali eneo hilo ijengwe zahanati ili wananchi wasisafiri umbali mrefu.
Amesisitiza kuwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan anathamini sana uhifadhi na yeye ndiye Mhifadhi namba moja lakini kutokana na adha ya wananchi wanayopata kusafiri umbali wa zaidi ya kilomita 16 ameona ni vyema Zahanati ijengwe ili wananchi wahudumiwe kwa urahisi
Katika hatua nyingine, Waziri Balozi Dkt.Pindi Chana amewataka wananchi hao kuacha kusafisha mashamba kwa kutumia moto hali ambayo imekua chanzo cha moto pale unaposhindwa kudhibitiwa na kusababisha hasara .
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mufindi ambaye ni Diwani wa Kata ya Mninga, Mhe.Festo Mgina amesema anamshukuru sana Rais Samia Hassan kwa kukubali ombi la wananchi wa Mninga lililowasilishwa kupitia Halmashauri ya Mufindi na kusisitiza kuwa Zahanati hiyo itawapa ahueni wananchi wake waliosumbuka kwa muda mrefu.
” Tangu nchi hii ipate uhuru wananchi wangu wamekuwa wakilazimika kusafiri umbali mrefu ili kupata huduma za afya lakini kwa kitendo hiki cha Mhe.Rais kutupa eneo la ujenzi wa Zahanati, tunamuahidi tutaendelea kumpa ushirikiano zaidi, amesisitiza Mhe. Mgina