Katibu mkuu wizara ya maliasili na utalii ,Profesa Eliamani Sedoyeka akifungua mafunzo hayo jijini Arusha.
Baadhi ya washiriki wakiwa katika mafunzo hayo jijini Arusha .
………………………………….
Julieth Laizer,Arusha.
Katibu mkuu wizara ya maliasili na utalii ,Profesa Eliamani Sedoyeka amewataka Wataalamu wa Sekta ya Utalii nchini kutoka idara ya malikale kubuni mikakati itakayowezesha Sekta hiyo kuwa na tija katika kuongeza pato la Taifa,sambamba kugundua maeneo mengine ya vivutio zaidi.
Profesa Sedoyeka ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku mbili juu mkataba wa Urithi wa Dunia.
Profesa Sedoyeka amesema kuwa,lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo juu ya mkataba wa Urithi wa Dunia ukihusisha wataalamu mbalimbali kutoka sekta ya utalii ambapo Tanzania inaungana na nchi mia moja sitini na saba duniani katika utekelezaji wa mkataba huo.
Aidha Sedoyeka amewataka wataalamu kuhakikisha wanaweka mikakati kuifanya Idara ya malikale inakuza uchumi wa nchi na kuongeza maeneo ya utalii zaidi.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Idara ya Malikale Dkt. Christowaja Ntandu amesema kuwa, umuhimu wa wataalamu kutoka idara ya malikale kupatiwa mafunzo kuhusu mkabata wa Urithi wa Dunia pamoja na kuweza kujua majukumu
yao katika kuhifadhi maeneo ya vivutio vya malikale kama urithi wa Taifa.
Nao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wamesema kuwa, mafunzo hayo ni muhimu kwani itasaidia kuongeza wigo wa utunzaji na uhifadhi wa utalii kwa maslahi ya kizazi cha sasa na kijacho,sambamba na kuongeza njia mbadala kwa Taifa kuongeza fedha za kigeni.
Aidha hadi kufikia januari mwaka 2023 maeneo 1157 yameingia kwenye orodha ya Urithi wa Dunia na Tanzania ikiwa na maeneo saba tu hivyo wadau na wataalamu kuweka juhudi ili kukngeza idadi hiyo kwa kufanya tafiti zaidi.