Mjumbe wa Kamati kuu ya Halmshauri kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Mlezi wa CCM Mkoa wa Pwani, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Pwani Mwinshehe Shaban Mlao wakati alipowasili Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere – Kibaha kuzungumza na Viongozi pamoja na Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi ikiwa ni Shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 46 ya CCM.
Mjumbe wa Kamati kuu ya Halmshauri kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Mlezi wa CCM Mkoa wa Pwani, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akipanda mti katika eneo la Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere Kibaha mkoani Pwani wakati alipowasili kuzungumza na Viongozi pamoja na Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi ikiwa ni Shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 46 ya CCM.
Mjumbe wa Kamati kuu ya Halmshauri kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Mlezi wa CCM Mkoa wa Pwani, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akisaini kitabu cha wageni alipowasili Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere Kibaha mkoani Pwani kuzungumza na Viongozi pamoja na Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi ikiwa ni Shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 46 ya CCM.
Mjumbe wa Kamati kuu ya Halmshauri kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Mlezi wa CCM Mkoa wa Pwani, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akihutubia Viongozi pamoja na Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani katika kuadhimisha Miaka 46 ya CCM hafla iliofanyika leo tarehe 04 Februari 2023 katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere Kibaha mkoani Pwani.
Mjumbe wa Kamati kuu ya Halmshauri kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Mlezi wa CCM Mkoa wa Pwani, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akipanda mti katika eneo la Shule ya Sekondari Tumbi iliopo Kibaha mkoani Pwani ikiwa ni Shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 46 ya CCM.
Mjumbe wa Kamati kuu ya Halmshauri kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Mlezi wa CCM Mkoa wa Pwani, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akiwa katika picha ya pamoja na walimu na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Tumbi iliopo Kibaha mkoani Pwani mara baada ya kupanda miti shuleni hapo ikiwa ni Shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 46 ya CCM.
.……………………………………….
Mjumbe wa Kamati kuu ya Halmshauri kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Mlezi wa CCM Mkoa wa Pwani, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango amewataka viongozi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi kutambua jukumu walilonalo katika taifa la kuwatetea wananchi, kusikiliza changamoto na kuzipatia ufumbuzi.
Dkt. Mpango amesema hayo wakati akihutubia Viongozi na Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani ikiwa ni shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 46 ya Chama Cha Mapinduzi hafla iliofanyika leo tarehe 04 Februari 2023 katika Ukumbi wa Shule ya Uongozi wa Mwalimu Nyerere iliopo Kibaha Mkoani Pwani. Amesema dhumuni la kuazishwa kwa chama hicho ni kutetea na kuwasemea wanyonge hivyo kinapaswa kukemea maovu na uonevu, kuwasemea wananchi na kubeba ajenda za wananchi kuanzia ngazi ya Shina hadi Taifa.
Aidha Makamu wa Rais amewasihi Viongozi wa Chama, Wabunge na madiwani kufanya kazi kwa karibu na pia kuisimamia Serikali kuwajibika ipasavyo katika utekelezaji wa Ilani ya CCM ikiwemo miradi yote inayotekelezwa kwenye Mikoa yao. Pia amewataka viongozi kutenga muda wa kuwasilkiiza wananchi waliowachagua kwa unyenyekevu kwa kutambua kwamba uongozi ni dhamana.
Dkt. Mpango ameiagiza Wizara ya Nishati kupitia TANESCO kuhakikisha wanashirikiana na wananchi kutatua kero zote zitokanazo na ujenzi wa miradi ya Nishati mkoani Pwani ikiwa ni pamoja na kulipa wananchi fidia stahiki na kwa wakati.
Aidha Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango amewapongeza wanachama na viongozi wa CCM mkoa wa Pwani kwa kuendelea kujiimarisha kiuchumi ikiwa ni pamoja kuanzisha miradi inayosaidia katika uendeshaji wa chama hicho mkoani Pwani. Ameeleza kwamba siasa safi zinaendana na uchumi imara hivyo amewasihi kuendelea kubuni vyanzo vipya vya mapato na kufanya uwekezaji wenye tija. Amesema ni muhimu kuendelea kugharamia uchaguzi kwa fedha za chama ili kuepuka kupata viongozi wenye maslahi binafsi katika uongozi wao.
Amewasihi wananchama wote wa CCM Mkoa wa Pwani kujiepusha na migogoro na makundi ndani ya chama pamoja na kuwaagiza kuongeza ushirikiano baina ya chama na serikali. Amewataka kuendelea kufanya siasa safi na kulinda amani na usalama wa nchi kwa kutoa taarifa kwenye vyombo husika kuhusu viashiria vyovyote vya uvunjifu wa amani.
Amewataka viongozi wa CCM Pwani kuendelea kuongeza wanachama na kuhimiza ulipaji wa ada za uanachama ili kuwezesha chama kujiendesha bila utegemezi.
Makamu wa Rais amewataka viongozi wa CCM mkoa wa Pwani kuzungumza na wanachama na wananchi wa mkoa huo athari kubwa zinazotokana na uharibifu wa mazingira ili kuchukua hatua za pamoja za haraka. Pia amesisitiza suala la ufugaji wa tija ili kuepukana na migogoro ya mara kwa mara ya wakulima na wafungaji pamoja na uharibifu wa mazingira. Amewasihi wanachama na wananchi wa Mkoa wa Pwani kuchukua hatua ya upandaji miti ikiwemo ya biashara na matunda ili kuendelea kulinda mazingira.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Pwani Abdallah Mwinyi amesema Chama hicho kinalenga kuendelea kujiimarisha kiuchumi kwa kutekeleza miradi mbalimbali ili kiweze kujiendesha. Amesema tayari ipo mipango ya muda mrefu , wa kati na muda mfupi ikiwemo umaliziaji wa jengo la kitega uchumi na ofisi za Chama hicho lililopo Kibaha.
Katika Maadhimisho hayo Makamu wa Rais ameshiriki zoezi la upandaji miti katika shule ya Sekondari Tumbi iliopo Kibaha mkoani Pwani na kuwasisitiza wanafunzi wa shule hiyo kuweka mkazo katika elimu kwa manufaa yao na taifa kwa ujumla. Pia amewataka wanafunzi hao kushiriki kikamilifu katika utunzaji mazingira kwa kuhamasisha wazazi na walezi katika maeneo yao kupanda miti.