Mbunge wa Geita Vijijini Dkt.Joseph Kasheku Msukuma akizungumza kwenye Maadhimisho ya miaka 46 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi CCM yaliyofanyika katika uwanja wa Furahisha uliopo Wilaya ya Ilemela Jijini Mwanza
Wananchi mbalimbali waliohudhuria kwenye Maadhimisho ya miaka 46 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi CCM yaliyofanyika katika uwanja wa Furahisha uliopo Wilaya ya Ilemela Jijini Mwanza
………………………………………….
Na Hellen Mtereko,Mwanza
Mbunge wa Geita Vijijini Dkt.Joseph Kasheku Msukuma, amesema mfumuko wa bei unaitesa sana Tanzania kutokana na bidhaa mbalimbali kuuzwa kwa bei ghari ukiwemo mchele.
Dkt.Msukuma ameyasema hayo leo Jumamosi Feburuari 4,2023 wakati akizungumza kwenye Maadhimisho ya miaka 46 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) yaliyofanyika katika uwanja wa Furahisha uliopo Wilaya ya Ilemela Jijini Mwanza.
Amesema ni vyema Serikali iliangalie suala hilo kwa jicho la tatu ili wananchi waweze kupata unafuu wa maisha kwakununua vyakula kwa bei nafuu.
Akizungumzia suala la kuwapanga wamachinga katika maeneo rafiki yatakayowafanya wafanye biashara zao kwa amani na utulivu Dkt.Msukuma, ameiomba Serikali ihamishe Shule ya Msingi Sahara iliyopo Wilaya ya Nyamagana ili wajenge machinga Complex ambayo itawaweka Wafanyabiashara hao pamoja hatua itakayosaidia kuondokana na changamoto ya kwenda nje ya mji ambayo inapelekea kufilisika kwa mitaji yao.
“Hakuna kitu kinaniumiza kichwa kama kuwaondoa wamachinga mjini suala la machinga limekuwa gumu hapa Mwanza ndio maana nimeamua kutoa mawazo yangu kwa kumuomba Rais wa Jamuhri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu kutenga eneo hilo la Shule ili machinga waweze kufanya biashara zao katika maeneo ya mjini”, amesema Dkt.Msukuma