Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM Taifa Mkoa wa Mwanza Jamal Babu akizungumza baada ya kupanda miti kweye Shule ya Sekondari Buzuruga
Muonekano wa vyumba vya madarasa Shule ya Sekondari Buzuruga iliyoko katika Wilaya ya Ilemela Jijini Mwanza
Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM Taifa Mkoa wa Mwanza Jamal Babu akiwa ameshika mti kwaajili ya kupanda kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari Buzuruga iliyoko katika Wilaya ya Ilemela Jijini Mwanza.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt.Angelina Mabula akitoa rai kwa wananchi kutunza miti inayopandwa katika Taasisi mbalimbali
……………………………………………….
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM Taifa (MNEC) Mkoa wa Mwanza Jamal Babu amesema dhamira ya CCM ni kuona Mkoa huo unaendelea kuwa wa kijani kwa kupanda miti katika taasisi mbalimbali hatua itakayosaidia utunzaji wa mazingira kuwa rafiki pamoja na upatikanaji wa mvua.
Ameyasema hayo leo Jumamosi Feburuari 4,2023 wakati alipokuwa akipanda miti kwenye Shule ya Sekondari Buzuruga iliyoko katika Wilaya ya Ilemela ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya miaka 46 ya kuzaliwa kwa Chama hicho Mkoani Mwanza.
“Moja ya Majiji ambayo yanatikiwa kuwa ya kijani ni Mwanza,Tanga na Pemba hivyo tujitahidi sana kuitunza hii miti ambayo inapandwa katika taasisi mbalimbali ili iweze kuboresha mazingira ya Shule”, amesema BabU.
Babu amesema miti ina umuhimu mkubwa sana katika Taifa hivyo jamii inapaswa kuwa na utaratibu wa kutunza miti kuanzia kweye ngazi ya familia.
“Tumekuwa tukipanda miti katika taasisi mbalimbali ili kuendelea kuifanya Mwanza kuwa ya kijani pia nawaomba sana wananchi muendelee kutunza miti kuanzia kweye kaya zenu hatua itakayosaidia kuachana na tabia ya ukataji wa miti kiholela.