Na Erick Mungele-DODOMA
Mkuu wa Mkoa wa Dododma Mhe Rosemary Senyamule amewataka watendaji wa kata za Viwandani, Chadulu, Makole na Hazina kuhakikisha wanafatilia wanafunzi ambao hawajaripoti shule wakahakikiwe kama wamefika shuleni hata kama wapo shule binafsi ili mradi wawe shule.
Ameyesema hayo,leo Februari 03,2023 jijini Dodoma katika shule ya sekondari Viwandani wakati akikagua maendeleo ya wanafunzi walioripoti shuleni pamoja na kuzungumza na watendaji wa kata hizo kutokana na shule hiyo kuwa na wanafunzi wa chache waliolipoti.
Aidha amewakata watendaji kuendelea kutekelez sera ya kukijanisha Dodoma nakuhimiza kila kaya kuweza kupanda miti na taasi zote zinazozungukia kata yake na kuhimiza kupanda kwa kupendezesha yaani kwa mpangilio.
“Nendeni mkahakiki nakuleta ripoti ya wanafunzi ambao bado hawajafika shule kwa kata zote na kwa shule binafsi kuhakikisha taarifa zao kama wameenda shule cha muhimu mwanafunzi awe shule hata kama yupo shule binasfi haina tatizo.
“Pia mnawajibu wakuendelea kuwaambia wanachi kuhusiana na srla ya kukijanisha dodoma kwa kila kaya na taasisi zote na kwakila kaya wanatakiwa kupanda miti wala 5 kwa kaya na kuhakikisha wanapanda kwa kupendezesha yaani kwa mpangilio”,amesema.
Aidha amewahimiza usafi wa mazingira kwa wanachi ili kuweka jiji safi na mazingira kwa ujumla na ambaye hatatekeleza sheria hiyo atatozwa faini hivyo kila mwananchi fanya usafi kila Jumamosi ya usafi.
Mhe.Senyamule ameshiriki pia katika zoezi upandaji miti katika shule hiyo yote ni kuendeleza utekelezaji wa kukijanisha Dodoma
Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa Kata ya Viwandani Tumi Dachi amemwaomba Mkuu wa mkoa kuweza kuwasaidia wanafuzni kuwaondolea wafanya biashara waliozunguka shule kuweza kuwaondoa maana wanawachanganya wanafunzi.