Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Profesa
Joyce Ndalichako, akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi PSSSF wakati
akilizindua Baraza la Pili mjini Morogoro Februari 2, 2023
NA
MWANDISHI WETU, MOROGORO
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe.
Prof. Joyce Ndalichako, ameupongeza Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa
Umma (PSSSF) kwa kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan la kulipa wastaafu mafao kwa wakati.
Prof.Ndalichako
ameyasema hayo leo Februari 2, 2023 mjini Morogoro alipokuwa akizindua Baraza
la pili la wafanyakazi wa mfuko wa PSSSF.
“Mlitumie
baraza hili kuhimiza kila mfanyakazi ajue wajibu wake ili kuuwezesha mfuko
kusonga mbele katika kutekeleza maagizo ya serikali pamoja na kutoa huduma bora
kwa wanachama,”amesema.
Aidha,
amesema Mhe.Rais ameendelea kushughulikia changamoto za wastaafu ikiwa ni
pamoja na kuwataka watendaji wa mifuko ya hifadhi ya jamii kulipa mafao
watumishi walioondolewa kazini kwa kubainika kuwa na vyeti feki.
“Kulikuwa
na jumla ya watumishi Elfu Kumi na Nne (14,000) ambao waliondolewa kwenye
utumishi kwa sababu ya vyeti feki, tayari watumishi 6,892 wameshalipwa na 3,169
bado madai yao yanafanyiwa kazi,” Alifafanua.
Awali,
Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA
Hosea Kashimba, amesema kwasasa mafao hayo ya wastaafu wanalipwa ndani ya siku
60 na uhakiki wa wastaafu unafanyika kidigitali.
Akitoa
taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Mfuko kwa nusu mwaka toka Julai 2022 hadi
Desemba 2022, CPA Kashimba alimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada kubwa aliyofanya ya kuhakikisha watanzania
wengi wanapata ajira.
“Tumevuka
lengo la kuandikisha wanachama kwa asilimia 270%, lengo letu lilikuwa
kuandikisha wanachama 13,000, lakini tumevuka lengo hilo na kuandikisha
wanachama 33,534, sisi wanachama wetu wanategemea jinsi serikali inavyoajiri,
watu wengi wameajiriwa katika kipindi hicho.” Alisema.
Eneo
lingine ambalo Mfuko umefanya vizuri ni makusanyo ya Michango ambapo lengo
lilikuwa ni kukusanya Shilingi Bilioni 792 lakini Mfuko umeweza kukusanya
Shilingi Bilioni 823 na hivyo kuvuka lengo kwa asilimia 104%.
Kuhusu
mapato yatokanayo na uwekezaji unaotokana na vitega uchumi, CPA Kashimba
alisema Mfuko uliweka lengo la kukusanya Shilingi Bilioni 256 na badala yake
Mfuko umeweza kukusanya Shilingi Bilioni 297 na hivyo kuvuka lengo kwa asilimia
116%.
Baraza
hilo linalofanyika kwa siku mbili, limechagua viongozi wapya wakiwemo Katibu wa
Baraza Bw. Steven Biko na Katibu Msaidizi Linda Njoolay.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (aliyesimama) akizungumza wakati akizindua Baraza la Wafanyakazi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kwenye ukumbi WA Magadu mjini Morogoro Februari 2, 2023. Kushoto ni Mwenyekiti wa Baraza hilo ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA Hosea Kashimba na kulia ni Katibu wa Baraza, Steven Biko.
Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi PSSSF, ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu, CPA Hosea Kashimba akizungumza wakati wa uzinduzi wa baraza hilo
wa Utawala na Rasilimali Watu, (PSSSF), Bw. Paul Kijazi.