WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dk. Stergomena Tax,akishuhudia wakati bendera ya Taifa la Ufaransa ikipandishwa kuashiria kuzinduliwa kwa Ofisi ndogo ya Ubalozi wa Ufaransa jijini Dodoma hafla iliyofanyika leo Januari 31,2023 .
Balozi wa Ufaransa nchini Mheshimiwa Nabil Hajlaoui akimkaribisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax alipowasili eneo la Kilimani jijini Dodoma kwa ajili ya kufungua rasmi Ofisi ndogo ya Uwakilishi ya Ubalozi wa Ufaransa katika makao makuu tarehe 31 Januari 2023
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dk. Stergomena Tax,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Ofisi ndogo ya Ubalozi wa Ufaransa jijini Dodoma hafla iliyofanyika leo Januari 31,2023.
Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Nabil Hajloui,akielezea malengo ya kufungua Ofisi ndogo ya Ubalozi wa Ufaransa jijini Dodoma hafla iliyofanyika leo Januari 31,2023.
Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) Bi.Celine Robert,akizngumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ofisi ndogo ya Ubalozi wa Ufaransa jijini Dodoma iliyofanyika leo Januari 31,2023
Mkurugenzi wa mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) Bw.Orivier Terra ,akizngumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ofisi ndogo ya Ubalozi wa Ufaransa jijini Dodoma iliyofanyika leo Januari 31,2023.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule,akielezea jinsi watakavyoshirikiana na balozi mbalimbali zitakazohamia Dodoma wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ofisi ndogo ya Ubalozi wa Ufaransa iliyofanyika leo Januari 31,2023.a
Sehemu ya wageni waalikwa wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dk. Stergomena Tax (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa Ofisi ndogo ya Ubalozi wa Ufaransa jijini Dodoma hafla iliyofanyika leo Januari 31,2023.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akiwa na Balozi wa Ufaransa nchini Mheshimiwa Nabil Hajlaoui akizindua rasmi Ofisi ndogo ya Uwakilishi ya Ubalozi wa Ufaransa katika eneo la Kilimani jijini Dodoma
Balozi wa Ufaransa nchini Mheshimiwa Nabil Hajlaoui akiagana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax baada ya kukamilika kwa hafla ya uzinduzi wa Ofisi ndogo ya Uwakilishi ya Ubalozi wa Ufaransa jijini Dodoma tarehe 31 Januari 2023
……………………………..
Na Alex Sonna-DODOMA
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dk. Stergomena Tax,amezindua Ofisi ndogo ya Ubalozi wa Ufaransa jijini Dodoma ikiwa ni sehemu ya kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia .
Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa ofisi hiyo leo Januari 31,2023 jijini Dodoma Waziri Tax amesema kuwa tukio hilo ni sehemu ya jitihada zinazofanywa na Rais Samia katika kuimarisha ushirikiano wa kimataifa.
Dk. Tax amesema kuwa serikali ya awamu ya sita imekuwa ikifanya jihada mbalimbali katika kuimarisha ushirikano na mataifa mbalimbali pamoja na masuala ya kidiplomasia.
“Leo hii tumekuwa na tukio la ufunguzi wa ofisi ya kuanzia ya ubalozi wa Ufaransa hapa Dodoma tunawashukuru sana kwa tukio hili lakini haya ni matokeo ya Rais Samia na jitihada zake za kutaka kuimarisha ushirikiano na mataifa mbalimbali na kurahisisha mawasiliano kati ya serikali yetu na mataifa mengine”amesema Dk.Tax
Aidha Waziri Tax amewataka mabalozi kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya sita kuhamia makao makuu Dodoma kwa kuanzisha ofisi zao na serikali itakuwa mstari wa mbele kutoa ushirikiano kufanikisha jambo hilo.
“Niwahakikishie kuwa serikali kupitia wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki itaendelea kutoa ushirikiano mtakao uhitaji muda wote lakini pia kwa Balozi ambazo zitakuwa tayari kutaka kufungua ofisi zao jijini Dodoma tutazisaidia kufanya hivyo”almesema Dk.Tax
Hata hivyo Dk. Tax almesema serikali inatambua jitihada mbalimbali za kimaendeleo ambazo zimekuwa zikifanywa na Ubalozi huo nchini katika sekta za nishati,maji pamoja na usafirishaji.
Awali Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Nabil Hajloui, amesema ufunguzi wa ofisi hiyo ni matunda ya Rais Samia Suluhu Hassan alipotembelea ofisi ya ubalozi huo alipofanya ziara mwaka jana nchini Ufaransa.
”Mataifa ya Tanzania na Ufaransa yamekuwa na ushirikiano wa kidiplomasia kwa muda mrefu hivyo kufunguliwa kwa ofisi hiyo ndogo jijini Dodoma kutaendeleza kuimarisha mahusinano yaliyopo kimataifa.”amesema Mhe.Hajloui