Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa umma na Utawala Bora Mhe.Jenista Mhagama,akizungumza wakati akifungua kikao cha kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya maadili na utawala bora kilichofanyika leo Januari 30,2023 jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa umma na Utawala Bora Mhe.Jenista Mhagama,akisisitiza jambo kwa washiriki wakati akifungua kikao cha kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya maadili na utawala bora kilichofanyika leo Januari 30,2023 jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa umma na Utawala Bora Bw.Xavier Daud,akizungumza wakati wa kikao cha kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya maadili na utawala bora kilichofanyika leo Januari 30,2023 jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Usimamizi Maadili kutoka, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa umma na Utawala Bora Bi.Leila Mavika,akitoa utangulizi wa kikao cha kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya maadili na utawala bora kilichofanyika leo Januari 30,2023 jijini Dodoma.
Sehemu ya washiriki wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa umma na Utawala Bora Mhe.Jenista Mhagama (hayupo pichani),wakati akifungua kikao cha kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya maadili na utawala bora kilichofanyika leo Januari 30,2023 jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara ya Mipango Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa umma na Utawala Bora Bw.Cosmas Ngangaji,akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasmi (hayupo pichani) mara baada ya kufungua kikao cha kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya maadili na utawala bora kilichofanyika leo Januari 30,2023 jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa umma na Utawala Bora Mhe.Jenista Mhagama,akiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari mara baada ya kufungua kikao cha kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya maadili na utawala bora kilichofanyika leo Januari 30,2023 jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa umma na Utawala Bora Mhe.Jenista Mhagama,akiwa katika picha ya pamoja na washiriki mara baada ya kufungua kikao cha kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya maadili na utawala bora kilichofanyika leo Januari 30,2023 jijini Dodoma.
PICHA ZOTE NA ALEX SONNA
……………………………………
Na Alex Sonna-DODOMA
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi na Utawala bora, Jenista Mhagama, ameagiza wadau wa usimamizi wa maadili katika utumishi wa umma kujadili kwa kina na kutoa mapendekezo kuhusu sababu za taasisi za umma kuendelea kuwa na viashiria vya uvunjifu wa maadili.
Agizo hilo amelitoa leo Januari 30,2023 jijini Dodoma wakati akifungua kikao cha kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya maadili na utawala bora,Mhagama amesema maeneo hayo matano yanayolalamikiwa zaidi kwa kukithiri kwa viashiria vya uvunjifu wa maadili.
“Kufanya utafiti ni kazi moja na kutoa matokeo ya utafiti ni Jambo lingine, hivyo hakikisheni unapokea taarifa,mkayabaini yaliyoko kwenye tafiti hizo na kuyafanyia kazi,”amesema
Hata hivyo Waziri Mhagama amesema kuwa kiwango cha uzingatiaji wa maadili katika utumishi wa umma kwa mwaka huu kimeongezeka hadi kufikia asilimia 75.9 ikilinganishwa na uliofanyika mwaka 2014 ambao kiwango kilikuwa asilimia 66.1.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Xavier Daud, amesema kuwa kikao hicho ni utekelezaji wa maagizo ya Waziri Mhagama aliyetaka kiitishwe ili kufanya majadiliano ya kina kuhusu matokeo ya utafiti huo na kuja na mikakati ya ufuatiliaji wa uzingatiaji wa maadili katika sekta zote kulingana na matokeo.
Awali, Mkurugenzi wa usimamizi maadili wa Ofisi hiyo, Leila Mavika, amesema utafiti huo ulilenga kuangalia wananchi Wanaridhika na huduma wanazopata, na kama watumishi wanaotoa huduma wanatimiza wajibu wao, ili serikali ichukue hatua stahiki.
Naye Mkurugenzi wa Idara ya Mipango kutoka ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Cosmas Ngangaji,akitoa neno la shukrani amesema kuwa wataenda kusimamia utumishi wa umma Kwa kutumia Sera, mifuko na usimamizi wa rasilimali watu katika Utumishi wa umma, watafikia malengo na matarajio ya Serikali na utaratibu huo lazima ushuke mpaka ngazi ya familia.