Pia kuelekea Ibada ya Hija mwaka huu,baraza hilo limeandaa utaratibu mzuri kwa waumini wa dini hiyo ya kiislamu watakaojaliwa kwenda kuhiji hvyo wafuate utaratibu huo kupitia BAKWATA kitengo cha Hija.
Akizindua mpango huo wa pili wa kujenga vituo vya Afya wa Mlango kwa Mlango wilayani Ilemela leo,Sheikhe wa Mkoa wa Mwanza,Alhaji Sheikhe Hasani Kabeke amesema unalenga kupata fedha za kukamilisha baadhi ya miradi.
“Wito wangu kwa waislamu na wasio waislamu watuunge mkono ili kukamilisha miradi hiyo inayogusa maisha na afya za wananchi wa dini zote na wasio na dini,kiu na dhamira yetu ni kuiunga mkono na kuisaidia serikali katika sekta ya afya kuhudumia wananchi,”amesema.
Sheikhe Kabeke amesema Wilaya ya Ilemela imekamilisha jengo la wagonjwa wa nje (OPD),Sengerema wamekamilisha boma na wanahitaji mabati zaidi ya 180 (bandol 11) na Misungwi wamekamilisha kuchimba msingi.
Sheikhe huyo wa mkoa amesema miradi hiyo ya afya itajengwa na asitokee wa kuzuia,katu waislamu wasikubali kugawanywa na watu wenye nia ya kukwamisha maendeleo ya jamii ya Waislamu na kuwarudisha nyuma,wahakikishe wanapigana kwa mikono miwili ikamilike wananchi wapate huduma.
Aidha kuhusu Ibada ya Haji,Sheikhe Kabeke amesema kupitia kitengo cha hija wameandaa utaratibu utakaowezesha waumini kwenda kutekeleza ibada hiyo muhimu na moja ya nguzo za Uislamu ikiwezekana kila wilaya ipate hujaji mmoja.
Amewataka wachanje chanjo ya homa ya ini, Uviko-19 na wawe na hati za kusafiria ambapo usafiri ni Dola za Marekani 6,000 na kuwashauri watakao kwenda hija hasa wafanyabiashara wawe na nguvu pamoja na afya njema.
Kwa upande wake Diwani wa Kirumba (CCM) Wessa Juma,amesema waislamu hawana budi kuchangia dini ya,wasipofanya hivyo hawawezi kujichangia wenyewe binafsi na kuwashawishi kufanya biashara na Mungu,wamkopeshe atawalipa.
“Serikali ina mkakati wa kujenga vituo vya afya kila kata,waislamu jambo hili la vituo vya afya si la sheikhe wa mkoa ni wajibu wetu sote na nitaendelea kuunga mkono shughuli za maendeleo ya dini yangu na jamii,hata India wanaishi kwa utaratibu huo,”amesema.