Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe. David Kihenzile akizungumza wakati wa Semina kwa Wabunge wa Kamati ya Viwanda, Biashara na Mazingira na Kamati ya Katiba na Sheria kuhusu Usimamizi wa Biashara ya Kaboni iliyofanyika leo Januari 27, 2023 katika Ukumbi wa Msekwa jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Andrew Komba akiwasilisha mada kuhusu namna biashara ya kaboni inavyofanyika wakati wa semina kwa wabunge kutoka Kamati ya Viwanda, Biashara na Mazingira na Kamati ya Katiba na Sheria Kaboni iliyofanyika leo Januari 27, 2023 katika Ukumbi wa Msekwa jijini Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi wa Huuduma za Sheria Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Kyamani Mugisha akiwasilisha mada kuhusu usimamizi wa biashara ya kaboni wakati wa semina kwa wabunge wa Kamati ya Viwanda, Biashara na Mazingira na Kamati ya Katiba na Sheria Kaboni iliyofanyika leo Januari 27, 2023 katika Ukumbi wa Msekwa jijini Dodoma.
Wabunge wa Kamati ya Viwanda, Biashara na Mazingira na Kamati ya Katiba na Sheria wakiwa katika Semina kuhusu usimamizi wa biashara ya kaboni iliyofanyika leo Januari 27, 2023 katika Ukumbi wa Msekwa jijini Dodoma.
Wajumbe wa Menejimenti ya Ofisi ya Makamu wa Rais wakifuatilia Semina kuhusu usimamizi wa biashara ya kaboni kwa wabunge Kamati ya Viwanda, Biashara na Mazingira na Kamati ya Katiba na Sheria iliyofanyika leo Januari 27, 2023 katika Ukumbi wa Msekwa jijini Dodoma.
Baadhi ya Wabunge wakichangia katika Semina kuhusu usimamizi wa biashara ya kaboni kwa wabunge Kamati ya Viwanda, Biashara na Mazingira na Kamati ya Katiba na Sheria iliyofanyika leo Januari 27, 2023 katika Ukumbi wa Msekwa jijini Dodoma.
(PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS)
****************************
Ofisi ya Makamu wa Rais imetoa semina kwa wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kuhusu Usimamizi wa Biashara ya Kaboni leo Januari 27, 2023 katika ukumbi wa Msekwa jijini Dodoma.
Katika semina hiyo mada mbili zimetolewa kwa wabunge hao ili kuwajengea uelewa wa masuala ya biashara ya kaboni ambayo tayari kanuni na mwongozo wa usimamzi umetolewa na Serikali.
Akizungumza wakati wa semina hiyo Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe. David Kihenzile amepongeza Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kuandaa semina hiyo kwani imekuwa na tija kwa wajumbe wa kamati hizo mbili.
Pia ameipongeza Ofisi hiyo kwa kukamilisha kanuni na mwongozo wa biashara hiyo ambayo inaweza kusaidia katika upatikanaji wa mapato katika halmashauri zenye misitu.
Katika semina hiyo wabunge wamepata wasaa wa kujifunza kuhusu mabadiliko ya tabianchi yanavyoleta madhara kwa taifa letu na duniani kwa ujumla na namna biashara ya kaboni inavyoendeshwa katika kukabiliana na athari hizo.
Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Andrew Komba ambaye aliwasilisha mada hiyo alitoa wito kwa wananchi kuendelea kuhifadhi misitu iliyopo katika maeneo yao ili kuweza kunufaika na biashara ya kaboni.
Pia Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Sheria Bw. Kyamani Mugisha alifafanua mbele ya wabunge wa kamati hizo kuhusu Kanuni na Mwongozo wa Biashara ya Kaboni ambao umetolewa hivi karibuni na kutangazwa katika Gazeti la Serikali.