Meneja wa benki ya NMB Tawi la Mirerani Allan Kombe (katikati) na wadau na watumishi wa benki hiyo wakiwa kwenye picha ya pamoja kwenye tafrija ya wiki ya huduma kwa wateja.
Watumishi wa benki ya NMB Tawi la Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wakiwa kwenye maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja.
Meneja wa benki ya NMB Tawi la Mirerani, Allan Kombe (kushoto) akiwa na wadau na watumishi wa benki hiyo kwenye tafrija ya wiki ya huduma kwa wateja.
*******************************
Na mwandishi wetu, Mirerani
Wafanyakazi wa benki ya NMB Tawi la Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wamezindua wiki ya huduma kwa wateja kwa kutangaza mpango mpya wa mikopo ya ‘Afya Loan’.
Meneja wa NMB Tawi la Mirerani, Allan Kombe akizungumza na wadau na wafanyakazi wa benki hiyo kwenye tafrija ya wiki hiyo alisema Afya Loan ni huduma mpya maalum ya mikopo kwa watu au taasisi binafsi.
Kombe alisema Afya Loan ina lengo la kuwakopesha wadau binafsi wenye maduka ya dawa, maabara, zahanati na vituo vya afya vya watu binafsi.
Alisema lengo la kuanzishwa kwa mikopo hiyo ya ‘Afya Loan’ ni kwa ajili ya kuimarisha huduma hizo za afya zinazotolewa na watu binafsi au taasisi binafsi.
“Mpango huo wa ‘Afya Loan’ utakuwa endelevu na wiki hii ya huduma kwa wateja itaendelea kwa mud wote wa mwezi huu wa Octoba,” alisema Kombe.
Ofisa Tarafa ya Moipo, Joseph Mtataiko aliwapongeza wafanyakazi wa benki ya NMB Tawi la Mirerani kwa kutoa huduma zao ipasavyo kwa wateja wanapofika kupata huduma za kibenki.
Mtataiko alisema watumishi wa serikali, wafanyabiashara, wakulima, wafugaji, wachimbaji madini na watu wa kada zote za Mirerani wanaopata huduma kwenye benki hiyo wanapongeza huduma nzuri zinazotolewa na benki hiyo.
Meneja wa huduma kwa wateja wa benki ya NMB Tawi la Mirerani, Bahati Nelson aliwakaribisha wadau wote wa benki hiyo kufika ofisini kwao ili wapatiwe huduma.
Bahati alisema benki ya NMB Tawi la Mirerani ipo pembeni ya barabara kuu ya Mirerani-Okresumet mbele kidogo ya kituo cha polisi Mirerani.