Msaidizi wa Askofu KKT Dayosisi ya Kaskazini Mchungaji Deogratius Msanya,akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Shule za Sekondari za Makanisa ulioandaliwa na Christian Social Services Commission (CSSC) unaofanyika kwa siku mbili kuanzia leo Januari 24 mpaka 25,2o23 jijini Dodoma.
Sehemu ya washiriki wakifatilia hotuba ya mgeni rasmi Msaidizi wa Askofu KKT Dayosisi ya Kaskazini Mchungaji Deogratius Msanya (hayupo pichani) wakati akifungua Mkutano wa Shule za Sekondari za Makanisa ulioandaliwa na Christian Social Services Commission (CSSC) unaofanyika kwa siku mbili kuanzia leo Januari 24 mpaka 25,2o23 jijini Dodoma.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Marangu Mwalimu Fredrick Matery,akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasm Msaidizi wa Askofu KKT Dayosisi ya Kaskazini Mchungaji Deogratius Msanya (hayupo pichani) mara baada ya kufungua Mkutano wa Shule za Sekondari za Makanisa ulioandaliwa na Christian Social Services Commission (CSSC) unaofanyika kwa siku mbili kuanzia leo Januari 24 mpaka 25,2o23 jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Christian Social Services Commission (CSSC) Bw.Peter Maduki,akielezea umuhimu wa Mkutano wa Shule za Sekondari za Makanisa ulioandaliwa na Christian Social Services Commission (CSSC) unaofanyika kwa siku mbili kuanzia leo Januari 24 mpaka 25,2o23 jijini Dodoma.
Mkuu wa Idara ya Elimu Baraza la Maskofu Tanzania (TEC) Sister Joyce Mboya,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufunguliwa kwa Mkutano wa Shule za Sekondari za Makanisa ulioandaliwa na Christian Social Services Commission (CSSC) unaofanyika kwa siku mbili kuanzia leo Januari 24 mpaka 25,2o23 jijini Dodoma.
Mkuu wa Shule ya Agape Lutheran Junior Seminary Mchungaji Godrick Lyimo,akizungumzia mikakati iliyopo katika shule za Makanisa katika kuwalea na kuwajenga kiimani wanafunzi mara baada ya kufunguliwa kwa Mkutano wa Shule za Sekondari za Makanisa ulioandaliwa na Christian Social Services Commission (CSSC) unaofanyika kwa siku mbili kuanzia leo Januari 24 mpaka 25,2o23 jijini Dodoma.
Msaidizi wa Askofu KKT Dayosisi ya Kaskazini Mchungaji Deogratius Msanya akiwa katika picha ya pamoja na washiriki mara baada ya kufungua Mkutano wa Shule za Sekondari za Makanisa ulioandaliwa na Christian Social Services Commission (CSSC) unaofanyika kwa siku mbili kuanzia leo Januari 24 mpaka 25,2o23 jijini Dodoma.
………………………………….
Na Alex Sonna-DODOMA
WAKUU wa shule za Sekondari za Makanisa nchini wametakiwa kusimamia maadili ya wanafunzi na walimu ili kuzalisha kizazi kiadilifu kitakachokuja kulisaidia Taifa katika miaka ya baadae.
Hayo yameelezwa leo Januari 24,2023 jijini Dodoma na Msaidizi wa Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini,Mchungaji Deogratius Msanya wakati akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa wakuu wa shule hizo ulioandaliwa na Christian Social Services Commission (CSSC).
Mch. Msanya amesema jambo kubwa linalosumbua kwa sasa ni maadili kwa wanafunzi na walimu hivyo kuna haja ya wakuu hao kusaidia kwa vitendo ikiwa ni pamoja na kupaza sauti.
“Lazima tukubali ambaye amejengwa kiimani na kimaadili atakuwa vizuri na atakuwa na hofu ya Mungu na hata mahali pa kazi utaona utendaji kazi wake,utakuwa ni wa hali ya kujali na ataonesha kuwajali wale anaowahudumia.
“Niseme ni jambo linasikitisha taasisi za kidini zikitajwa jambo la msingi ni kufanyia kazi na kuthibitisha isije ikawa ni mambo ambayo ya kufikirika.
“Kama yapo mambo ambayo sio mazuri tuchukue hatua za haraka kushughulika tatizo hilo kwa sababu tutakuwa na kizazi chenye shida,”amesema Mch.Msanya
Hata hivyo ameishauri Serikali kutafuta ufumbuzi wa kero mbalimbali ambazo zinajitokeza katika jamii ikiwemo suala la ukosefu wa maadili na vitendo ambavyo havimpendezi Mungu.
“Changamoto naona ni utandawazi taarifa zipo kiganjani wanafunzi wanajifunza mambo mengi sana, watoto kuwapa simu wakiwa na umri mdogo nayo ni shida.
“Ukweli tungependa sana shule zetu zisitajwe kwenye mambo kama hayo wakuu wa shule zetu angalieni elimu yenye maadili,”amesema Mchungaji huyo.
Amesema kwa upande wa shule za serikali haina mzaha na wao wanapashwa kusimamia kwa umoja wetu kupinga mambo ambayo hayampendezi Mungu.
Kwa upande wake,Mkurugenzi Mtendaji wa Christian Social Services Commission (CSSC), Bw.Peter Maduki amesema taasisi hiyo ilianzishwa mwaka 1992 kwa ajili ya kuimarisha huduma za utoaji wa elimu na afya zinazotolewa na taasisi za makanisa.
Amesema wana taasisi za elimu 1033 ambazo zimesajiliwa na serikali katika ngazi ya elimu ya awali msingi,sekondari vyuo vya kati, ufundi na Vyuo Vikuu.
Amesema lengo ni la kuhakikisha tunatoa elimu bora kwa watu wote kwa usawa hasa wale wenye changamoto mbalimbali ili mhusika aelimike kiakili na kiroho.
“Mpaka sasa kuna mafanikio tuna taasisi nyingi za elimu zenye ubora na vijana wanafaulu vizuri katika masomo yao.
“Ili kufikia lengo la kufaulu huwa tunatoa mafunzo ya mara kwa mara kwa walimu wetu ili wawe mahiri tukishirikiana na Serikali,”amesema Maduki.
Amesema ili elimu iwe bora wanashughulikia suala la maadili kwa kufuata sera ya ulinzi wa mtoto na kufundisha elimu ya dini kwa wanafunzi na mafunzo ya kanuni za kazi na maadili kwa walimu ili kuhakikisha wanafunzi wanalelewa katika misingi ambayo wanatarajiwa na jamii.
“Tunatoa mafunzo kwa watoto kujitambua na kujilinda, walimu na wazazi pamoja na jamii inayowazunguka kwamba ulinzi wa mtoto unaanzia nyumbani,” amesema
Amesema wanajaribu kuimarisha mafunzo ya dini ili wanafunzi waishi kulingana na maadili na wanakuwa na upendo kuwaepusha kwenda kinyume na msingi wa kanisa.
“Tumenzisha klabu za ulinzi wa Watoto mashuleni ili waweze kuelimishana juu ya mambo hayo.Wito wangu kwa jamii, malezi lazima yahusishe jamii nzima malezi mazuri yanatolewa wasiwkuelimishana juu ya mambo hayo. Wito wangu kwa jamii na wazazi, malezi lazima yahusishe jamii nzima malezi mazuri yanatolewa nyumbani wasiwaachie walimu peke yao,”amesema amesema Maduki.
Naye Mkuu wa Idara ya Elimu Baraza la Maskofu Tanzania (TEC) ,Sister Joyce Mboya ,amesema kupitia mkutano huo wamejifunza kuhusu malezi kwa vijana na watahakikisha shule wanazozisimamia kwa vitendo.
“Ndio maana sisi tuna sera inayotuongoza na tuna vitabu vya kufundishia ili wakienda popote waweze kufanya kazi wawe wawajibikaji na wabunifu kwa ajili ya kuendeleza Taifa,”amesema Mboya.