Naibu Waziri wa Afya Godwin Mollel mwenye suti nyeusi akipokea msaada wa vifaa tiba kutoka kwa Afisa mkuu huduma shirikishi kutoka benki ya NMB ,Nenyuata Mejooli
Naibu Waziri wa Afya ,Godwin Mollel akizungumza katika halfa ya kukabithi vifaa tiba vilivyotolewa na benki ya NMB kwa ajili ya kusaidia vituo viwili vya afya jijini Arusha.
Mbunge wa Arusha mjini, Mrisho Gambo akizungumza katika halfa hiyo jijini Arusha
………………………………….
Julieth Laizer ,Arusha.
Arusha.Benki ya NMB imekabithi msaada wa vifaa tiba vyenye dhamani ya shs 26 milioni katika kituo cha afya Mkonoo na Levolosi kwa ajili ya kusaidia upatikanaji bora wa huduma za afya katika vituo hivyo.
Aidha vifaa vilivyokabithiwa ni vitanda 10 vya kujifungulia wakinamama pamoja na vitanda 10 vya kulazia wagonjwa wa kawaida kwa kituo cha afya Mkonoo huku mabenchi 20 yakitolewa kwa ajili ya wagonjwa wanaosubiria kupata huduma katika kituo cha afya cha Levolosi .
Afisa mkuu huduma shirikishi kutoka benki ya NMB ,Nenyuata Mejooli akizungumza wakati wa kukabithi vifaa hivyo amesema kuwa,wao kama wadau wanaunga mkono juhudi za serikali kwa kusaidia maswala mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni njia mojawapo ya kurudisha faida wanayoipata kwa jamii.
Amesema kuwa, benki hiyo imejikita zaidi katika kutoa elimu ya afya pamoja na majanga mbalimbali kwa ustawi wa maendeleo ya nchi yetu.
Kwa upande wa Naibu waziri wa afya Dkt,Godwin Mollel akipokea msaada huo amesema kuwa, kitendo kilichofanywa na benki hiyo kinapaswa kuigwa na wadau mbalimbali kwani kwa kufanya hivyo wanaiunga mkono serikali katika juhudi za kusukuma maendeleo.
Mollel amesema kuwa, serikali inafanya mambo mengi sana ya maendeleo ambapo inakuwa ni changamoto kufikia kila mahali ila wanapotokea wadau kama hao kusaidia ni jambo nzuri sana kwani kwa pamoja wanamuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan.
Aidha amemwomba DMO wa kituo hicho cha afya pindi wanaopata fursa ya kupeleka wauguzi masomoni atoe kipaumbele kwa manesi wa kituo hicho ili nao waweze kunufaika na fursa hiyo.
Kwa upande wake Mbunge wa Arusha mjini,Mrisho Gambo amesema kuwa, kituo hicho cha afya kata ya Mkonoo bado kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya vifaa tiba ,nyumba za watumishi,mashine ya X-ray ,kifaa cha kuchomea taka, hivyo wameiomba wizara ya afya kukiangalia kituo hicho kwa namna ya kipekee kwani kinahudumia wananchi wengi kutoka maeneo mbalimbali.
Gambo amesema kuwa,wanashukuru sana kwa msaada huo uliotolewa na benki hiyo ambapo ameomba kuongezwa kwa vitanda vingine kwani hivyo havitoshi kulingana na mahitaji yaliyopo.
“Tunaomba upatikanaji wa dawa katika kituo hiki cha afya uwe wa uhakika sio mgonjwa akija kupata huduma ya dawa anakutana na aspirin na panadol peke yake,tunaomba sana wizara ya afya izingatie jambo hili ili wananchi waweze kufurahia huduma zote katika kituo hiki.”amesema Gambo.
Baadhi ya wananchi wakizungumza katika eneo hilo wameshukuru serikali kwa kuwapatia kituo hicho kwani kimeleta manufaa makubwa sana kwao kutokana na umbali mrefu waliokuwa wanatembea kaa ajili ya kufuata huduma za afya,ambapo waliomba wadau mbalimbali kuendelea kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kusaidia vifaa tiba kituoni hapo.