Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Mhe.Selemani Jafo,akizungumza katika ufunguzi wa kikao kazi cha kuwaapisha wakurugenzi wapya jijini Dodoma katika ukumbi wa Mikutano Video Conference katika Ofisi za TAMISEMI .
Naibu Katibu Mkuu OR-TAMISEMI anayeshughulikia Elimu Ndugu. Mathias Kabunduguru,akiongea katika ufunguzi wa kikao kazi cha kuwaapisha wakurugenzi wapya jijini Dodoma katika ukumbi wa Mikutano Video Conference katika Ofisi za TAMISEMI .
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Mhe.Selemani Jafo,akisisitiza jambo kwa wakurugenzi wapya wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha kuwaapisha wakurugenzi wapya jijini Dodoma katika ukumbi wa Mikutano Video Conference katika Ofisi za TAMISEMI .
Sehemu ya wakurugenzi wapya wakifatilia ufunguzi wa kikao kazi cha kuwaapisha wakurugenzi wapya jijini Dodoma katika ukumbi wa Mikutano Video Conference katika Ofisi za TAMISEMI .
Wakurugenzi wapya wakiapo cha uadilifu likiendelea.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Mhe.Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na wakurugenzi wapya mara baada ya kufungua kikao kazi cha kuwaapisha wakurugenzi wapya jijini Dodoma katika ukumbi wa Mikutano Video Conference katika Ofisi za TAMISEMI .
PICHA NA ALEX SONNA-FULLSHANGWEBLOG
……………………..
Na.Majid Abdulkarim,
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Mhe.Selemani Jafo, amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri nchini kusimamia mapato na kuwa wabunifu katika kubuni vyanzo vya mapato ili kufikia uchumi wa kati.
Hayo yamebainishwa leo katika ufunguzi wa kikao kazi cha kuwaapisha wakurugenzi wapya jijini Dodoma katika ukumbi wa Mikutano Video Conference katika Ofisi za TAMISEMI .
Waziri Jafo amesema kuwa kila kiongozi aloteuliwa anadhamana kubwa ya kwenda kuwatumikia watanzania kwa kuwaletea maendeleo kwa kusimamia vyema vyanzo vya mapato na miradi husika katika eneo lake la kazi.
“Hakikisheni kila mradi unaotekelezwa katika malmaka ya serikali za mitaa unaendana na ubora wa kiwango cha fedha za mradi husika ili kuonyesha uhai wako katika nyazi yako ulonayo hapo katika kituo chako cha kazi” amesema Waziri Jafo
Waziri Jafo ameendelea kwa kutoa wito kwa viongozi hao kwa kuwataka kuwa wabunifu katika kubuni vyanzo vya mapato katika maeneo yao ya kazi ili kufikia kuinua uchumi wa halmashauri moja moja na taifa kwa ujumla.
Lakini pia Waziri Jafo. amewataka kuwa na mahusiano mazuri na wakuu wa idara na watumishi wanao waongoza ndo itakuawa njia yenye baraka katika kuleta chachu ya maendeleo katika mamlaka za serikali za mitaa.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu OR-TAMISEMI anayeshughulikia Elimu Ndugu. Mathias Kabunduguru amewataka viongozi hao kuhakikisha mapato yanyopatikana katika mamlaka za serikali za mitaa yanawezesha wananchi wake katika kukuza uchumi wan chi kwa kuwatengenezea mazingira mazuri ya kuanzisha viwanda vidogo vidogo, kujihusisha katika shughuli za kibiasha ndogo ndogo ili kuinua uchumi wa nchi.
Ndugu Kabunduguru amesema kuwa ili kutekeleza vyema majukum yao lazima kuwa waadilifu katika kulitumikia taifa ili kwani uandilifu kazini ndo msingi wa mtumishi wa umma.
“Kubwa ni kuwa na ushirikiano na watumishi unaowaongoza , kusikiliza wananchi unaowatumikia ili kufikia utekelezaji mzuri wa maendeleo katika mamlaka za serikali za mitaa kwani kila mmoja katika mamlaka hizo anamchango wake katika kuleta maendeleo ya taifa hili” amesema Ndugu Kabunduguru
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kibiti , Mohamed Mavura akizungumza kwa niaba ya Wakurugenzi wenzake amesema kuwa wamepokea maelekezo na sasa ni kuyafanyia kazi kwa ushirikiano wa hali ya juu na watumishi wanao waongoza ili kuendeleza pale walipoishia wenzao katika mazuri yote.
Ikumbukwe hivi karibuni Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amefanya uteuzi wa Wakurugenzi waypa katika Halmashauri kumi nchini.