Meneja mauzo kanda ya magahari Trifot Melkiory akingumza na waandishi wa Habari hawapo picha juu wa kampeni ya NMB MastaBata, Kote-Kote iliyofanyika kwenye Tawi la Benki Mihayo mkoani Tabora
Meneja mauzo kanda ya magahari Trifot Melkiory akipimpingia simu mteja wa aliyeshinda pikipiki kupitia kampeni ya wiki ya NMB MastaBata, Kote-Kote.
Mkaguzi wa bodi ya michezo ya kubahatisha Gooluck Msomiguw aliyevaa shati njeupe katika ni Meneja mauzo kanda ya magahari Trifot Melkiory na maafisa wengine wa benki hiyo wakishuhudia droo ikichezwa leo mkoani hapa.
Mtumishi wa chama kikuu cha wakulima wa Tumbaku Wetcu mkoani Tabora Emanuel Malumbo aliyevaa kadi jeusi akikabidhiwa kadi ya pikipiki aina ya boss na Meneja mauzo kanda ya magahari Trifot Melkiory huku kaimu meneja wa benki ya NMB tawi la Mihayo Prudence Kwenyemba akishuhudia tukio hilo .
Meneja mauzo kanda ya magahari Trifot Melkiory akimkabidhi ufungua wa Pikipiki Mtumishi wa chama kikuu cha wakulima wa Tumbaku Wetcu mkoani Tabora Emanuel Malumbo.
**************************
Na Lucas Raphael,Tabora
*MSHINDI WA WIKI ILIYOPITA AKABIDHIWA PIKIPIKI MPYA MKOANI HAPA
*AIDAN LUKINDO WA MOROGORO ACHUKUA PIKIPIKI KUKABISHIWA WIKI IJAYO.
Benki ya NMB nchini imetoa zaidi ya shilingi 200,000,000/- kwa washindi 713 katika wiki ya tano za kampeni ya MastaBata KoteKote inayondelea kwa sasa
Kauli hiyo ilitolewa na meneja mauzo kanda ya magahari Trifot Melkiory wakati akishuhudia droo ya tisa ya wiki ya kampeni ya NMB MastaBata, Kote-Kote iliyofanyika kwenye Tawi la Benki Mihayo mkoani Tabora.
Alisema kwamba wakati fedha hizo zikitolewa kwa washindi hao lengo nikutoa kiasi cha shilingi milioni 300 ambazo zitatolewa kama zawadi kwa washindi 854..
Melkiory alisema kwamba NMB wataendelea na droo ambayo itatoa washindi 75 wakijishindia shilingi laki moja moja na mshindi mmoja atapata pikipiki kila wiki
Meneja mauzo wa kanda hiyo aliendelea kusisitiza kwamba NMB wanaedelea kuhamasisha wateja matumizi ya kadi zao za NMB master card, sio tu kwa ajili ya kutolea pesa katika ATM bali katika matumizi mbalimbali kama kufanya malipo kwa lipa Mkononi katika sehemu za migahawa, supermarket, vituo vya mafuta.
Alisema kwamba malipo hayo yanaweza kufanyika hata katika sehemu za starehe na kuagiza bidhaa mbalimbali kupitia mitandao.
“Ilikupata nafasi ya kushinda zawadi hizi na kufanya msimu huu wa MastaBata kufana zaidi kwa wateja wetu. Wateja wetu wanapaswa kufanya miamala yao kupitia kadi ya NMB Mastercard au Mastercard QR mara nyingi iwezekanavyo kwani kila unapofanya muamala unajitengenezea nafasi ya kuibuka na zawadi.”alisema Melkiory
Hata hivyo droo wiki hii iliyofanyika leo mkoani Tabora mshindi wa pikipiki aliyeshida ni Aidan Lukindo mkazi wa mkoa wa Morogoro anayetumia tawi la wami na kuwapata washindi 75 wa shilingi laki moja kila moja .
Aidha benki hiyo pia ilikamkabidhi mtumishi wa chama kikuu cha wakulima wa Tumbaku Wetcu Emanuel Malumbo aliyeshida wiki iliyopita pikipiki mpya aina ya Boxer.
Malumbo aliishukuru banki hiyo kwa kuendesha droo na kufanikiwa kupata zawadi ya pikipiki ambayo itamsaidia kwenda kwenye shughuli zake za kila siku.