MASHABIKI wa ngumi mkoa wa Tanga wanatarajiwa kushuhudia pambano la ngumi la
kufungua mwaka 2023 wakati w mabondia Mustafa Doto kutoka Dar es Salaam
atakapopambana na Said Mundi kutoka Tanga katika mnyukano wa round 10 kesho
Januari 18, 2023.
Akizungumza na waandishi wa Habari Jijini hapa leo, Promota maarufu
nchini, Ali Mwazoa na ambaye pia mtayarishaji wa pambano hilo alieleza
kutakuwa na mengine ya utangulizi 9.
Mapambano hayo yatakuwa kati ya Jay Jay atakayepambana na Peter Julius wakati
Jonas Mtafya atapigana na Patrick Kimweri. Wengne ni Hamis Mwambashi
dhdi ya Haji Juma, wote kutoka Tanga.
Mtoto wa bondia mkongwe nchini, Rashid Matumla, Snake Junior atapambana na Ali
Reli wote kutoka Tanga..
Haya ni mapambano ya utangulizi kwa ajili ya mabondia chipukizi kuelekea
pambano kubwa la aina yake mkoani na nchini Tanzania kati ya mabondia wawili
wanaogopwa, Ibrahim Classic atakayemkabili bondia mwenye mikwara na ngumi
nzito, Ndondande Harmer, wa nchini Zimbabwe. Pambano hilo litakuwa la round
10.
Promota Mwazoa alitoa wito kwa mashabiki wa jijini Tanga na nje ya mkoa
kujitokeza kwa wingi kushuhudia mabambano hayo mawili yatakayofanyika 18 na 28
Januari ambayo yatautangaza mkoa katika fursa za biashara na ajira.
Pia Mwazoa aliahidi kuandaa mapambano mengine ya ngumi ambayo yatatoa zaidi
fursa kwa vijana wanaochipukia katika ulingo wa michezo ya ngumi nchini.