MAMLAKA
ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) amesema uorodheshwaji wa
hatifungani ya Benki ya KCB yaani KCB Fursa Sukuk, ni miongoni mwa
sehemu ya maendeleo katika sekta ya fedha hapa nchini na inaweka
historia ya kuwa hatifungani ya kwanza inayokidhi misingi ya Shariah
kutolewa kwa umma na kuorodheshwa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam,
na ambayo imeidhinishwa na Mamlaka hiyo.
Akizungumza
Januari 13,2023 jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kuorodheshwa
kwa hatifungani inayokidhi misingi ya shariah kwenye soko la hisa la Dar
es Salaam ,Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka hiyo Nicodemus Mkama amesema
Oktoba 25, 2022 CMSA ilidhinisha Benki ya KCB kuuza hatifungani
inayokidhi misingi ya shariah.
“Yaani KCB Fursa Sukuk, yenye
thamani ya Sh. bilioni 10 na ongezeko la Sh.bilioni 5.Idhini ilitolewa
na CMSA baada ya Benki ya KCB kukidhi matakwa ya Sheria ya Masoko ya
Mitaji na Dhamana Sura ya 79 ya Sheria za Tanzania. Pia na Miongozo ya
Masoko ya Mitaji na Dhamana ya Utoaji wa Hatifungani ya mwaka 2019
ambapo pamoja na mambo mengine, KCB ilitakiwa kuwa, Waraka wa Matarajio
wa utoaji wa hatifungani ya Fursa Sukuk.
“Kuidhinishwa na Bodi ya
Ushauri wa Shariah (Shariah Advisory Board) ya benki ya KCB na kupata
ithibati kutoka kwa kampuni yenye utaalam kuhusu uwekezaji unaokidhi
Misingi ya Shariah.Benki ya KCB ilikidhi matakwa haya kwa kuwa na Bodi
ya Ushauri wa Shariah ambayo ni KCB Sahl Shariah Advsory Board na
ithibati ilitolewa na Kituo cha ushauri kuhusu uwekezaji unaokidhi
Misingi ya Shariah.”
Amesema Mauzo ya hatifungani ya Fursa Sukuk yalifunguliwa Novemba 9, 2022 na kufungwa Desemba 5 , 2022, ambapo kiasi.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA),CPA Nicodemus Mkama