*********************
Mtumba-Dodoma
Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) amefanya ziara maalumu ya Kutembelea na kukagua Mradi wa Ujenzi wa Jengo la Ofisi za Wizara ya Maji lililopo katika Eneo la Mtumba Mkoani Dodoma Linalogharimu Zaidi ya Tsh Billioni 22.9
Katika Ziara hiyo Mhe. Waziri ameishukuru serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutekeleza zoezi la ujenzi wa majengo ya ofisi za Wizara zote na hususani Ofisi ya Wizara ya Maji yenye Jengo lenye uwezo wa kuhudumia zaidi ya watu 518 na hivyo kuleta ufanisi kwa watumishi katika utendaji wao wa kazi.
Aidha Mhe. Waziri amempongeza Mkandarasi anayejenga mradi huo kwa kufanya kazi nzuri na kwa kasi na muda sahihi ambapo mpaka Sasa mradi umefikia asilimia 82 huku zikibaki asilimia 18 tu ili mradi huo uweze kukamilika.
Huu ni mwendelezo wa desturi alioanza nayo Waziri Aweso katika kuusimamia na kuufuatilia mradi huu tangu hatua za mwanzo kabisa hadi sasa akiwa na malengo ya kuona unakamilika kwa wakati na kwa viwango ambapo amekua akitembelea kujionea hatua za ujenzi mara kwa mara na amekiri hatua hii iliofikiwa imekidhi matarajio na matamanio yake.