**************************
NA FARIDA MANGUBE MOROGORO.
Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za mitaa,(TAMISEMI) Anjela Kairuki amewatahadharisha watumishi wa umma wanaokiuka taratibu na kanuni za kiutumishi kwa kutoa lugha chafu kwa wananchi huku akiahidi kuwashughulikia.
Waziri Kairuki ametoa kaiuli hiyo mkoni Morogoro akizungumza na walimu katika kikao kazi cha cha uboreshaji wa usimamizi wa elimumsingi na sekondari, kilichowakutanisha maafisa elimu Wilaya na Kata, wakuu wa shule za sekondari, na walimu wakuu wa shule za msingi mkoani humo.
Alisema wapo watumishi wanaotoa lugha chafu na zinarekodiwa na kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii, hiyo sio sawa, na Serikali ya Awamu ya sita inayoongozwa na Rias Dk. Samia Suluhu Hassan haiwezi kumvumilia mtumishi asiye na nidhamu mahala pakazi.
“Ili kudhibiti hali hii tumeweka mitego kila sehemu zinapotolewa huduma za kijamii ili kuwabaini wenye tabia za kutoa lugha chafu na sambamba mitandaoni ili tuwachukulia hatua.” Alisema Waziri Kairuki.
“Watu tunaowaweka ni maalumu sio wananchi hivyo watawatega kwa maswali ili mjibu lugha chafu tuwabaini, lile lililotokea kwa watumishi wa afya hivi karibuni Tabora sio wale tu wapo wengi”aliongeza.
Akizungumzia kuhusu masuala ya rushwa kazini Waziri Kairuki alisema wapo baadhi ya watumishi wanaotoa rushwa ili kupata madaraka jambo ambalo ni kinyume na taratibu za kiutumishi.
Alisema hategemei kama mkuu wa shule ameingia kwa kutoa rushwa atafanya kazi kwa uadilifu, maana lazima atafanya kila njia ili aweze kurejesha kike alichotoa.
” Kama mambo haya yapo yakome mara moja, Serikali ipo makini, hatutawafumbia macho wote watakaobainika watachukuliwa hatua”alisema.
Akitoa salamu za Mkoa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Bi. Fatma Mwasa alisema Septemba, 2022, Mkoa huo ulipokea Fedha kutoka Serikali Kuu kiasi cha shilingi bilioni sita na milioni mia tisa (6,900,000,000.00) kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 345 ili kuwapokea Wanafunzi wa Kidato cha Kwanza 2023 ambapo madrasa 336 yamekamilika na 3 yapo katika hatua za mwisho.
Alisema Mkoa wa Morogoro umeandikisha wanafunzi wa Darasa la Awali 70,872 wakiwemo wavulana 34,708 na wasichana 36164, mpaka sasa wanafunzi 65,786 wamekwisha andikishwa wakiwemo wavulana 32,543 na Wasichana 33,243 sawa na aslilimia 93.
Darasa la Kwanza wanafunzi waliotarajiwa kuandikishwa ni 78,846 wakiwemo wavulana 39,195 na wasichana 39,651, walioandikishwa hadi kufikia tarehe 06/01/2023 ni 74,578 Kati yao Wavulana ni 37,342 na Wasichana ni 37,578 sawa na asilimia 94.5 ambapo Miongoni mwa wanafunzi hawa walioandikishwa wamo wenye mahitaji maalum.
kwa mwaka wa fedha wa 2021/2022, mkoa wa Morogoro umepokea kiasi cha shilingi 5,640,000,000.00 kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya 12 za Sekondari katika Kata ambazo hazikuwa na shule za Sekondari na zile zenye wanafunzi wengi ukilinganisha na miundombinu ya Shule zilizopo.