*********************
MKUU wa Wilaya ya Nyasa Mh. Aziza Mangosongo amezindua wiki maalum ya upandaji miti katika Wilaya ya Nyasa ambapo jumla ya miti ya asili 3500 imepandwa.
Uzinduzi wa zoezi hilo umefanyika katika Chanzo cha maji cha Likwilu kilichopo katika Kijiji cha Likwilu Kata ya Kilosa Wilayani ya Nyasa.
Katika chanzo Hicho jumla ya miti ya asili 300 aina ya migwina, imepandwa wakati wa uzinduzi wa kampeni hii na jumla ya miti million moja na laki tano inatarajiwa kupandwa katika msimu huu wa kilimo ifikapo mwezi mei 2023. ya Upandaji Miti
Mkuu wa Wilaya wa Wilaya ya Nyasa amesema wilaya inatekeleza maagizo ya kuhifadhi vyanzo vya maji, kama yalivyotolewa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ambapo kwa kuanzia amesema wameamua kupanda miti kwenye chanzo cha maji cha Likwilu na kuendelea kwenye vyanzo vyote vya maji na mito yote inayoingiza maji kwenye Ziwa Nyasa.
Akizungumza baada ya kuzindua upandaji miti kwenye chanzo cha maji cha Likwilu Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Nyasa, aliyewakilishwa na Kaimu Katibu Tawala Wilaya ya Nyasa Ndugu Paul Lugongo, amekitaja chanzo hicho kuwa kina umuhimu mkubwa kwa wakazi wa Kata ya Kilosa kwa kuwa ni chazo cha kutegemewa cha maji safi yanayotumiwa na wakazi wa Kata hiyo.
Amewaagiza Viongozi wa Kata na Vijiji kuhakikisha kuwa,vyanzo vyote vya maji vinahifadhiwa na kutunzwa na kuhakikisha mifugo yote haifungwi katika chanzo cha maji.amwewataka Viongozi hao kuwahamasisha wananchi wapande miti na kutunza mazingira.
Awali akisoma Taarifa fupi kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Nyasa, Afisa Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira Wilaya ya Nyasa Bugingo Bugingo amesema,lengo la Halmashauri ni kupanda miti million moja laki tano kila mwaka,na wananchi Wilayani Nyasa wamehamasika kulima kilimo cha miti kwa kuwa wanapata faida kubwa baada ya kuuza mazao ya misitu.
Kwa upande wao wanmanchi waliohudhuria wamesema wamehamasika kulima kuhifadhi vyanzo vya maji na kuhifadhi mazingira kwa kuwa wanaona jisi maji yanavyopungua na kupata adha ya umeme na maji.aidha wanakwenda kuwa mabalozi kwa wananchi wengine ambao hawakuhudhuria.
Imeandaliwa na Netho Sichali
Afisa Habari,Kitengo cha mawasiliano Serikalini
Wilaya ya Nyasa.