Mkurugenzi wa Yuhoma Education Limited Yusuph Yahaya
……………………………..
Na Hellen Mtereko,Mwanza
Wazazi wametakiwa kuwekeza kwenye kusomesha watoto ili waweze kuwasaidia pindi wanapozeeka kwani elimu ni akiba.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Yuhoma Education Limited Yusuph Yahaya, wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake zikiwa zimesalia siku chache shule zifunguliwe
Amesema baadhi ya wazazi wamekuwa wagumu kuwekeza katika elimu hali inayopekekea kuishi maisha magumu baada ya kuzeeka hivyo ni vyema kusomesha watoto ili waweze kupata dira ya maisha.
Yahya ameeleza kuwa wamekuwa wakijihusisha na utoaji wa ushauri wa elimu ikiwemo kuwashauri wazazi ni wapi watoto wao wasome ili waweze kukamilisha ndoto zao za baadae.
Kwa mwaka huu amesema wamejipanga vyema kupeleka watoto kusoma nje ya nchi kwani kwa sasa hali ya hewa ni nzuri vyuo vingi vinafanya kazi kutokana na nchi nyingi kufungua lockdown.
Amesema kwa sasa elimu imekuwa kipaumbele katika nchi ya Tanzania japo kunachangamoto ya ajira kikubwa mwanafunzi anatakiwa asome ili aweze kupata elimu itakayomsaidia kupambana na soko la ajira.
Mwisho alitoa rai kwa wazazi ambao hawataki kuwapeleka watoto shule waachane na hiyo dhana kwani kwa sasa elimu ndio uwekezaji wa pekee ambao utawasaidia kuondokana na umasikini.