****************
Bonanza la sikukuu ya Krismas lililoandaliwa na taasisi ya The Angeline Foundation kwa kushirikiana na ofisi ya mbunge wa jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula limefana kwa michezo na zawadi kwa wananchi wa jimbo hilo kama sehemu ya kusherekea sikukuu
Akizungumza katika viwanja vya Furahisha kata ya Kirumba mratibu wa bonanza hilo Bwana Fidelis Irengo Lubala amesema kuwa kila mwaka inapofika sikukuu ya Krismas Mbunge wa Jimbo hilo amekuwa na desturi ya kukutanisha wananchi wake na kusheherekea nao pamoja ambapo Kwa mwaka huu amegawa zawadi kwa watoto wadogo ikiwemo vifaa vya shule kama madaftari, kalamu, pamoja na mbuzi, mipira, kuku kanga na fulana kwa wakubwa sanjari na kuendesha mashindano ya kukimbiza kuku, mpira wa miguu, kucheza na kuimba Ili kuibua vipaji vipya na kuendeleza vile vya zamani
‘.. Lengo la Mbunge mbali na kusheherekea sikukuu lakini pia anatoa fursa kwa wananchi kuonyesha vipaji vyao na kuviendeleza ..’ Alisema
Aidha Fidelis akawata wananchi kuhakikisha wanaendelea kuunga mkono juhudi za Mbunge huyo Kwa kushiriki shughuli za maendeleo pamoja na kumuombea Ili aweze kuwatumikia
Kwa upande wake Afisa Michezo wa manispaa ya Ilemela Bwana Kizito Bahati Sosho amewaasa wazazi kuleta watoto wao katika mabonanza ya aina hii ambayo hayafundishi watoto maadili yasiyofaa badala yake yanatoa fursa ya watoto kujifunza Mambo ya msingi ikiwemo utaratibu uliowekwa wa kuuliza watoto maswali ya darasani na anaeshinda kupewa zawadi ya madaftari ambayo yatawasaidia shuleni
Amina Jackson ni miongoni mwa watoto walioshiriki bonanza hilo ambapo amempongeza Mbunge huyo na kumshukuru Kwa kuendesha mashindano Kwa watoto huku akiwata viongozi wengine kuiga mfano huo unaotoa fursa sawa Kwa watoto kujifunza na kusheherekea pamoja bila kujali tofauti zao