Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Adam Malima akizungumzia namna ambavyo machinga wanaacha kufanya biashara kwenye maeneo yao rasmi
Wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa wamachinga wakiwa kwenye kikao
********************
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Adam Malima amewataka viongozi wa machinga kuwaondoa wafanyabiashara wote wanaofanya biashara kinyume na sheria na taratibu katika maeneo yasiyo rasmi.
Kauri hiyo imekuja baada ya wamachinga kutoka kwenye maeneo yao waliyopangiwa na kuamua kuja kwenye maeneo yasiyo rasmi kwaajili ya kufanya biashara zao.
Malima ameeleza kuwa mji wa Mwanza unapaswa kuwa wa kitalii na wa kisasa endapo machinga wataendelea kufanya biashara zao kiholela bila mpangilio na kuacha maeneo rasmi waliopangwiwa hauwezi kuwa tena kama unavyoakiwa kuwa.
” Mimi nimekaa London Kwa muda mrefu na huko pia Kuna machinga wa aina zote lakini wanafata taratibu walizopangiwa na siku ya ratiba yao wanafungua mitaa ili machinga wafanye biashara zao iweje huku hawataki kukaa katika maeneo yao” alisema Malima.
Amewataka viongozi wa pande zote mbili (Shiuma na Muungano)kwenda kuzungumza na wafanyabiashara hao ili waondoke katika maneno hayo na kama Kuna tatizo lolote wanapaswa kwenda kumuona Mkuu wa Mkoa mwenyewe ili aweze kuwatatulia shida zao na sio kujichukulia sheria ya kwenda kufanya biashara katika maeneo ambayo sio rasmi.
Hata hivyo ametoa wito Kwa Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana na Mkurugenzi wa Jiji kuhakikisha wanatengenezea miundombinu rafiki katika maeneo yote rasmi waliyoyachagua Kwa ajili ya wafanyabiashara hao kufanyia biashara zao.