Afisa Mtendaji wa kata ya Lunguya Bw. Paschal Ezekiel Manhyakenda akizungumza wakati wa Mdahalo kuhusu mikakati ya kutokomeza ukatili wa kijinsia katika kata ya Lunguya Halmashauri ya Msalala.
Mwezeshaji kutoka Mtandao wa Jinsia (TGNP) Aluwa Hamisi Mkilindi akizungumza kwenye Mdahalo kwa ajili ya kujadili mikakati mbalimbali ya kutokomeza ukatili wa kijinsia katika kata ya Lunguya Halmashauri ya wilaya ya Msalala Mkoani Shinyanga.
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Imeelezwa kuwa vitendo vya Ukatili wa Kijinsia katika kata ya Lunguya Halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga vimepungua kwa kiasi kikubwa kutokana na kazi nzuri inayofanywa na Kituo cha Taarifa na maarifa kinachosimamiwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) pamoja na Kamati ya Mpango wa Kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto (MTAKUWWA).
Hayo yameelezwa Jumanne Desemba 20,2022 na Afisa Mtendaji wa kata ya Lunguya Bw. Paschal Ezekiel Manhyakenda wakati wa Mdahalo kuhusu mikakati ya kutokomeza ukatili wa kijinsia katika kata hiyo kilichohudhuriwa na viongozi wa ngazi ya kijiji, kata na makundi mbalimbali ya wanajamii.
Manhyakenda amesema Kituo cha Taarifa na Maarifa kata ya Shilela kimekuwa kikishirikiana vizuri na serikali katika kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia hali iliyosababisha kupungua kwa matukio ya ukatili pamoja na kuongezeka kwa kasi ya wananchi kutoa taarifa za vitendo ya ukatili.
“Kituo cha taarifa na maarifa kinafanya kazi nzuri. Najivunia pia kuwa na Kamati ya Mpango wa Kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto (MTAKUWWA) mahiri na inayofanya kazi vyema (active), hivi sasa vitendo vya ukatili wa kijinsia vimepungua na kumekuwa na ongezeko la utoaji taarifa za matukio ya ukatili”,ameeleza Manhyakenda.
“Tunawashukuru TGNP kwa kuendelea kushirikiana na serikali kutoa elimu ya masuala ya ukatili wa kijinsia. Elimu hii ilitakiwa itolewe na serikali lakini nyinyi mnaitoa. Nyinyi wananchi mliopata bahati ya kupata elimu hii naomba mkawe mbegu ya kusaidia jamii kujitambua na kuachana na vitendo vya ukatili wa kijinsia”,amesema Afisa Mtendaji huyo wa kata ya Lunguya.
Katika hatua nyingine amesema ili kutokomeza kabisa vitendo vya ukatili wa kijinsia ni lazima jamii ijitambue na kila mtu kumthamini mwenzake.
“Ukatili wa kijinsia upo kwa wote wanaume na wanawake, ili kukomesha ukatili ni lazima kila mmoja amthamini mwenzake. Usimfanyie mwenzio ukatili”,amesema.
Naye Mwezeshaji kutoka TGNP, Aluwa Hamisi Mkilindi amesema ukatili wa kijinsia utatokomezwa endapo kila mmoja atajisimamia na kuwa mlinzi wa mwenzake huku akisisitiza jamii kuvunja ukimya ‘kupaza sauti’ kwa kujitokeza kutoa taarifa ya vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Nao washiriki wa mdahalo huo wamesema mabadiliko yanayoonekana sasa yanayotokana na elimu ambayo imekuwa ikitolewa mara kwa mara na Kituo cha taarifa na maarifa Lunguya juu ya madhara ya ukatili wa kijinsia huku wakishauri pia wanaume wanaofanyiwa ukatili wa kijinsia wavunje ukimya na kutoa taarifa ili jamii iishi kwa amani.
Afisa Mtendaji wa kata ya Lunguya Bw. Paschal Ezekiel Manhyakenda akizungumza wakati wa Mdahalo kuhusu mikakati ya kutokomeza ukatili wa kijinsia katika kata ya Lunguya Halmashauri ya Msalala

Mwezeshaji kutoka Mtandao wa Jinsia (TGNP) Aluwa Hamisi Mkilindi akizungumza kwenye Mdahalo kujadili mikakati mbalimbali ya kutokomeza ukatili wa kijinsia katika kata ya Lunguya Halmashauri ya wilaya ya Msalala

Mshiriki wa mdahalo, Edson Furaha akizungumza kwenye Mdahalo kujadili mikakati mbalimbali ya kutokomeza ukatili wa kijinsia katika kata ya Lunguya Halmashauri ya wilaya ya Msalala
Washiriki wa Mdahalo wakipiga picha ya kumbukumbu
Picha na Kadama Malunde – Malunde 1 blog