Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Ilemela kimewataka viongozi wake kuwa mstari wa mbele katika kuchangia na kuhamasisha ujenzi wa ofisi za chama hicho kwa ngazi ya kata na matawi
Akizungumza wakati wa ziara ya kushukuru wajumbe Kwa kumchagua, kukagua uhai wa chama na kuhamasisha ujenzi wa ofisi za kata na matawi, Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ilemela Mhe Yusuph Bujiku amewataka viongozi waliochaguliwa kuhakikisha wanajenga ofisi pamoja na kuendelea kuisimamia Serikali
‘.. Tutumie dhamana tulizopewa kuimarisha chama, kujenga chama, Na sisi wa wilaya tutakuwa wakali kwa viongozi wazembe ..’ Alisema
Aidha Bujiku amewapongeza Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hasan kwa kuchaguliwa sanjari na kutekelezwa shughuli za maendeleo
Kwa upande wake Katibu wa CCM wilaya ya Ilemela Bi Aziza Isimbula amefafanua kuwa ni wajibu wa chama kuisimamia Serikali baada ya uchaguzi na kuhakikisha Ilani ya uchaguzi inatekelezwa wakati Diwani wa kata ya Kayenze Mhe Issa Mwalukila Dida akimshukuru Rais Mhe Dkt Samia kwa kutoa zaidi ya milioni 500 kwaajili ya shughuli za maendeleo ndani ya kata yake na kumpongeza Mbunge wa Jimbo hilo Dkt Angeline Mabula Kwa kuchaguliwa kuwa mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM taifa (NEC)
Nae Katibu Mwenezi wilaya ya Ilemela Bwana Kazungu Safari Idebe amehitimisha kuwa ziara hiyo ni matokeo ya upangaji safu ya CCM kuanzia matawi mpaka taifa baada ya kuisha Kwa uchaguzi hivyo kazi iliyobaki ni kupambana kuendelea kushika dola na kuwatumikia wananchi