*****************
Kiwanda cha Sukari Mtibwa kimepewa siku saba kuhakikisha kinaziba mto uliochepushwa kuelekea kwenye mashamba ya miwa bila ya kibali cha Bodi ya maji Bonde la Wami Ruvu.
Mwenyekiti wa Bodi ya maji ya bonde la wami ruvu Bi. Hafsa Matasiwa ameyasema hayo kwenye ziara iliyofanyika katika kiwanda hicho yenye lengo kukagua vyanzo vya maji.
Amesema mwezi julia mwaka huu bodi ilitoa barua ya kusitisha matumizi ya maji kwa wadau kutokana na upungufu wa mvua lakini kiwanda hicho hakikufuata maagizo yaliotolewa na bodi hiyo na kuendelea kuchepusha maji kwenye mashamba yao ya miwa.
“Kila mtu angechepusha huu mto tungekuwa hatuna jina la mto, ambacho tunaomba tunatoa siku saba hapa pafungwe kabisa bodi ya maji bonde la mto ruvu tunasema hapa pafungwe.” Alisema Mwenyekiti wa bodi ya maji bonde la wami ruvu.