Afisa Maendeleo ya Vijana Mwandamizi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Bi. Diana Kasonga akiwasilisha mada wakati wa mafunzo ya stadi za Maisha yaliyotolewa kwa wakufunzi na watendaji wa masuala ya Watu wenye Ulemavu yanayofanyika katika hoteli ya Midland, mkoani Mwanza
Sehemu ya wakufunzi na watendaji wa masuala ya Watu wenye Ulemavu wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa katika mafunzo hayo ya stadi za Maisha yanayoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu kupitia Idara ya Maendeleo ya Vijana.
Mwezeshaji wa Stadi za Maisha, Bw. Robert Semkiwa (aliyesimama) akiwasilisha mada kuhusu Kuepuka Shinikizo Rika wakati wa mafunzo hayo ya stadi za Maisha yaliyotolewa kwa wakufunzi na watendaji wa masuala ya Watu wenye Ulemavu yanayofanyika katika hoteli ya Midland, mkoani Mwanza,
Mwezeshaji wa Stadi za Maisha, Bi. Rhoda Kagogo (kushoto) akiwasilisha mada wakati wa mafunzo ya stadi za Maisha yanayofanyika mkoani Mwanza
Baadhi ya wakufunzi na watendaji wa masuala ya Watu wenye Ulemavu ambao pia ni Wawezeshaji Kitaifa wa Stadi za Maisha (National Facilitators) wakiwa katika sehemu ya maigizo wakati wa mafunzo hayo.
Wakufunzi na Watendaji wa masuala ya Watu wenye Ulemavu wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa katika mafunzo hayo ya stadi za Maisha yanayoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu kupitia Idara ya Maendeleo ya Vijana yanayofanyika mkoani Mwanza, Disemba 15, 2022.
*************************
Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu kupitia Idara ya Maendeleo ya Vijana inaratibu Programu ya Stadi za Maisha (Life Skills) kwa lengo la kuwawezesha vijana mbinu zitakazowapa uwezo wa kujiimarisha kiakili na kiujuzi ili kumbambana na uhalisia wa Maisha ya kila siku.
Idara hiyo yenye dhamana ya maendeleo ya vijana nchini imetoa mafunzo kwa wakufunzi na watendaji wa masuala ya Watu wenye Ulemavu ambao pia ni Wawezeshaji wa Stadi za Maisha Kitaifa (National Facilitators) ili kuhakikisha elimu hiyo inajumuishwa kwenye afua na program za kushughulikia changamoto za vijana wenye Ulemavu.
Aidha, Mafunzo hayo yanalenga kuwawezesha wakufunzi na watendaji hao elimu ya stadi za maisha inawafikia vijana wenye Ulemavu ili waweze kujitambua, kuwa na uthubutu na kufanya maamuzi sahihi na kuepuka vishawishi pamoja na mazingira hatarishi.
Vile vile, Stadi hizo za Maisha zitawaongezea hali bora ya vijana nchini na kuwawezesha kuwa watu wenye tija katika jamii zao, sambamba na kumwezesha kijana asiye na Ulemavu na wenye Ulemavu kupata majibu kwa maswali makuu matatu (3) ya maishani ambayo ni Mimi ni nani; Ninataka kwenda wapi maishani; na Nitafikaje huko ninakotaka kwenda.