Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu (Mb) Mhe. George Simbachawene akizungumza na wananchi katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika kata ya Mtera.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu (Mb) Mhe. George Simbachawene akikagua mradi wa ujenzi wa josho katika kijiji cha Mtera.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu (Mb) Mhe. George Simbachawene akimkabidhi baiskeli ya kutembelea Bwn. Ayubu Makaburi kwa ajili ya Mwanae Mwenye Ulemavu Yusuphu Ayubu.
……………………………………….
Na Mwandishi wetu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene ametoa rai kwa wananchi wa Mtera kuacha kutumia nyavu haramu katika shughuli zao za uvuvi.
Wito huo ameutoa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene katika Mkutano wa hadhara aliofanya kata ya Mtera jimbo la Kibakwe Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa uliolenga kusikiliza na kutatua kero za wananchi.
“Msitumie nyavu za timba; ambazo zina sumu, ambazo zinauwa mazalia ya samaki na hata kwa mtumiaji wa samaki, waliovuliwa kwa nyavu hizo anaathirika.”
Bwawa linashindwa kuwa endelevu kwa sababu hakuna shughuli za uvuvi zinazoendelea kutokana na kukosekana kwa samaki.
“Afisa Uvuvi wa Halmashauiri ya wilaya ya Mpwapwa kushirikiana na Maafisa uvuvi katika maeneo yanayozunguka bwawa la mtera muandae andiko ambalo litasaidia kuja na mkakati wa Uvuvi endelevu katika bwawa la Mtera,” alisema Waziri Simbachawene.
Hii Itasaidia kutengeneza vikundi vya wavuvi vitakavyopewa uwezeshaji, ili viweze kupita kwa wavuvi wenzao kuwaelimisha juu ya athari zinazotokea kutokana na wavuvi kutumia nyavu haramu.
Naye afisa Uvuvi wa Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa Bwn, Fransisco Mwanga amesema uvuvi wa kutumia nyavu haramu aina ya timba ni hatari, madhara yake inapogusana na samaki ni kushindwa kuzaliana.
Elimu imetolewa kwa wavuvi na wakati mwingine kupigwa faini lakini bado wameendelea na uvuvi haramu uliosababisha samaki kutozaliana”
“Akizungumzia tatizo la uvuvi haramu Bwn. Hussein Mkwizu amesema swala hilo linapaswa kuwa ajenda ya kudumu kwenye vikao vya maendeleo vya kijiji ili kuweza kujenga uelewa wa pamoja kwa wananchi.”
“Lazima kuwe na kikosi kazi kitakachohusisha wabunge wa Majimbo yote yanazonguka bwala la Mtera kitakachojikita katika kuelimisha umma.”
Hakuna kambi ambayo imezunguka bwawa la mtera ambayo haijapitia hiii shida, sasa hivi kila mtu anafikiria namna tatizo hili linavyoweza kutatuliwa na lisijiruide