WAZIRI wa Maliasili na Utalii Balozi Dk.Pindi Chana,akizungumza kabla ya kupokea Tuzo aliyopewa Rais Samia na Taasisi ya Kimataifa ya International Iconic Award ya nchini India na kukabidhiwa na Taasisi ya Miss Jungle International na Taasisi ya Bega kwa Bega na mama Foundation ya Muongoza watalii bora kupitia filamu ya ‘Tanzania The Royal Tour’ leo Desemba 11,2022 jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Juma Mkomi,akizungumza kwenye hafla ya kupokea Tuzo aliyopewa Rais Samia na Taasisi ya Kimataifa ya International Iconic Award ya nchini India na kukabidhiwa na Taasisi ya Miss Jungle International na Taasisi ya Bega kwa Bega na mama Foundation ya Muongoza watalii bora kupitia filamu ya ‘Tanzania The Royal Tour’ leo Desemba 11,2022 jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Miss Jungle International, Haroun Kinega,,akizungumza kwenye hafla ya kupokea Tuzo aliyopewa Rais Samia na Taasisi ya Kimataifa ya International Iconic Award ya nchini India na kukabidhiwa na Taasisi ya Miss Jungle International na Taasisi ya Bega kwa Bega na mama Foundation ya Muongoza watalii bora kupitia filamu ya ‘Tanzania The Royal Tour’ leo Desemba 11,2022 jijini Dodoma.
Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dk.Pindi Chana,akipokea tuzo kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe.Dk.Samia Suluhu Hassan aliyotunukiwa na Taasisi ya Kimataifa ya International Iconic Award ya nchini India ya kumtambua kuwa Muongoza watalii bora kupitia Filamu ya ”The Royal Tour’
…………………………….
Na Alex Sonna-DODOMA
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan,Tuzo ya kimataifa ya kuwa muongoza watalii bora nchini kutoka Taasisi ya Kimataifa ya International Iconic Award ya nchini India.
Akizungumza leo Desemba 11,2022 jijini Dodoma wakati wa kupokea tuzo hiyo kwa niaba ya Rais Samia,Waziri wa Maliasili na Utalii Dk.Pindi Chana,amesema Rais Samia ametambuliwa kuwa Muongoza watalii bora kupitia Filamu ya ”The Royal Tour”ambayo imetajwa kuleta ushawishi wa Kitalii nchini.
Dk. Chana, amesema kuwa Wizara hiyo inamshukuru Rais Samia kwa kuwaongoza kwenye filamu hiyo ambayo sekta mbalimbali zimenufaika na kufungua utalii nchini.
“Nampongeza Rais kwa kutunukiwa tuzo hii na kuwa muongoza watalii namba moja, na huu ni wakati wetu sisi kujipima kwenye kutangaza utalii, tuje na ubunifu wa aina mbalimbali ,”amesema Dk. Chana
Amesema kuwa sekta ya utalii imeongeza mauzo ya nje kwa asilimia 25, wastani asilimia 17.2 ya pato ghafi la taifa huku kuzalisha ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja ni milioni 1.5.
“Mchango wa sekta ya utalii unapaswa kuongezeka zaidi kulinganisha na vivutio vya utalii vilivyopo, tunashukuru Miss Jungle inakuja na mazao mapya ya kutangaza Tanzanite,”amesema
Aidha Waziri Chana ameeleza kuwa lengo ni kuongeza idadi ya watalii kufikia milioni tano na mapato ya dola za kimarekani Bilioni sita ifikapo mwaka 2025.
Tuzo hiyo tuzo hiyo imetolewa na Taasisi ya International Iconic Award ya nchini India na kukabidhiwa na Taasisi ya Miss Jungle International na Taasisi ya Bega kwa Bega na Mama Foundation.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Juma Mkomi, amewataka watendaji wa Wizara hiyo kuendelea kuongeza ubunifu katika kuhifadhi na kutangaza maeneo ya utalii yaliyopo.
Awali, Mwenyekiti wa Taasisi ya Miss Jungle International, Haroun Kinega, amesema kuwa filamu hiyo ni hatua ya kuichukua Tanzania kuipeleka duniani na kilichofuata ni kuileta dunia nchini Tanzania.