JAJI Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Juma,akikagua mabanda mbalimbali wakati wa Maadhimisho ya kilele cha siku ya Maadili na Haki za Binadamu kitaifa 2022 yaliyofanyika leo Desemba 10,2022 jijini Dodoma.
JAJI Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Juma,akizungumza na wananchi pamoja na viongozi mbalimbali wakati wa Maadhimisho ya kilele cha siku ya Maadili na Haki za Binadamu kitaifa 2022 yaliyofanyika leo Desemba 10,2022 jijini Dodoma.
WAZIRI wa Nchi-Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Jenista Mhagama,akizungumza wakati wa Maadhimisho ya kilele cha siku ya Maadili na Haki za Binadamu kitaifa 2022 yaliyofanyika leo Desemba 10,2022 jijini Dodoma.
KAMISHNA wa Maadili nchini Jaji Sivangilwa Mwangesi,akitoa maelezo ya utangulizi wakati wa Maadhimisho ya kilele cha siku ya Maadili na Haki za Binadamu kitaifa 2022 yaliyofanyika leo Desemba 10,2022 jijini Dodoma.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Jabir Shekimweri,akitoa salamu za Mkoa wa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule, wakati wa Maadhimisho ya kilele cha siku ya Maadili na Haki za Binadamu kitaifa 2022 yaliyofanyika leo Desemba 10,2022 jijini Dodoma.
SEHEMU ya washiriki wakifatilia hotuba ya Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Juma (hayupo pichani) wakati ,akizungumza na wananchi pamoja na viongozi mbalimbali kwenye Maadhimisho ya kilele cha siku ya Maadili na Haki za Binadamu kitaifa 2022 yaliyofanyika leo Desemba 10,2022 jijini Dodoma.
……………………………..
Na Alex Sonna-DODOMA
JAJI Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Juma,amewaonya watumishi wa umma wasiofuata misingi ya utawala bora katika kuteleleza majukumu yao.
Kauli hiyo imetolewa leo Desemba 10,2022 jijini Dodoma wakati akizungumza kwenye maadhimisho ya kilele cha siku ya Maadili na Haki za Binadamu kitaifa 2022.
Prof. Juma amesema kuwa kumekuwepo na vitendo vinavyoashiria ukiukwaji wa ahadi za uadilifu kwa upande wa viongozi na watumishi wa umma na sekta binafsi.
“Natoa wito kwa viongozi wote wanaosimamia utoaji huduma katika sekta ya umma na binafsi kuwajibika na kusimamia utoaji wa huduma bila kudai au kupokea rushwa.”amesema Prof.Juma
Aidha amewataka watumishi wa mahakama ngazi zote kuzingatia maadili na misingi kwa kuepuka vitendo vya rushwa kwa wananchi wanapotafuta haki.
“Tukumbuke kuwa, watumishi wa Umma wanaojihusisha na vitendo vya rushwa huwakosesha wananchi haki zao za msingi, ustawi wao, na wa Taifa. Kwa kufanya hivyo watambue kuwa, wanafanya vitendo vya kijinai, na pia, wanakiuka Haki za Binadamu na kwamba wanavunja Ibara ya 12 – 21 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977,”amefafanua Prof.Juma
Prof.Juma amesema kuwa rushwa isipodhibitiwa hujijengea mfumo wake usio rasmi ambao huumeza na kutokomeza mfumo rasmi.
“Kila kiongozi, mtumishi, mwananchi na wadau wote tuna wajibu wa kupinga na kukataa kila aina ya uovu katika jamii ikiwemo rushwa, uonevu, wizi, ubadhirifu wa mali na uvunjifu wa haki za binadamu”amesema
Kwa upande wake Waziri wa Nchi-Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.Jenista Mhagama,amesema kuwa mapambano dhidi ya rushwa nchini ni jukumu la kila mtu na siyo la serikali pekeyake.
”Serikali itaendelea kusimamia maadili na haki za binadamu kwa watumishi wanaoenda kinyume na haitawavumilia watumishi wa umma wanaosababisha kuvunja maadili na haki za binadamu.’amesema Waziri Mhagama
Naye Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Geofrey Pinda amesema wanalaani vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto na kwamba serikali haina huruma na watu wanaofanya hivyo na kwenye hilo hakuna sehemu ya kuponea na badala yake watachukuliwa hatua stahiki.
Awali akitoa maelezo ya utangulizi,Kamishna wa Maadili nchini Jaji Sivangilwa Mwangesi,amesema katika kuadhimisha siku ya Maadili na Haki za Binadamu mwaka huu shughuli mbalimbali zimefanyika.
Amesema kuwa wametoa elimu kwa kurusha vipindi maaalum vya runinga na redio vilivyotumika kuelimisha umma kuhusu maadili, haki za binadamu, utawala bora na mapambano dhidi ya rushwa.
”Tulitembelea gereza la Isanga na Msalato jijini Dodoma hapa lengo likiwa ni kuongea na kuwasikiliza wafungwa katika magereza yao na kutoa elimu kwa umma katika viwanja vya Nyerere squre ambapo jumla ya taasisi 16 zimeshiriki.’;amesema Jaji Mwangesi