Moyo alisema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Ikuvilo baada ya kubaini kuwa kuna baadhi ya watendaji wanapokea rushwa na matukio hayo hayafiki katika vyombo vya sheria.
Alisema kuwa suala lolote linalohusu masuala ya ukatili wa kijinsia suala hili lisilishughulikie na watendaji lipeleke kwenye vyombo vya sheria au polisi.
“Kuanzia sasa masuala yote yanayohusisha na ukatili wa kijinsia yakiletwa ofisini ya mtendaji wa kata yapelekwe polisi yakafayiwe kazi ikitokea mtendaji wa Kijiji ndio anafanya suluhu la jambo hilo atafunguliwa mashtaka”
Alisema kuwa wamegundua kuwa kuna baadhi ya watendaji wa kata na vijiji sio waaminifu wanashirikiana na baadhi ya wazazi katika matendo haya kwa kupewa rushwa na kukubali kuyamaliza bila kuyafikisha polisi.
Alieleza kuwa jambo hilo linasababisha wananchi kushindwa kutoa taarifa kwa kuogopa kutoa ushahidi mahakamani na kulinda ndugu wanaofanya uhalifu huo na kumalizana nyumbani.
Hali hiyo inapelekea waathirika wa ukatili kukosa haki yao ya msingi na wanawaweka katika hatari ya kupata maambukizi ya magonjwa mbalimbali.
Kwa upande wake Onesmo Mtove mkazi wa Kijiji cha Ikuvilo alisema kuwa wanaiomba serikali kuipa kipaumbele upatikanaji wa haki za kisheria katika matukio ya ukatili wa kijinsia.
“Kwa huku vijijini msaada wa kisheria bado ni changamoto kwa sababu huduma hizo ziko mbali tunaomba serikali isogeze ili wana vijijini tuweze kupata sehemu za kusemea na kupata msaada wa kisheria kwa haraka”alisema
Naye sarafina Mtega alisema kuwa jamii ielimishwe iachane na mil ana destuli zilizopitwa na wakati Pamoja na mfumo dume jambo ambalo linapelekea matukio hayo kuongezeka na wanawake kuendelea kuyavumilia bila kutoa taarifa.
“Jamii inapaswa kupewa elimu elekezi na wanaume waache mfumo dume ili wanawake wapate haki zao katika ngazi ya familia hili litasaidia sana kupunguza matukio ya ukatili wa kijinsia”alisema sarafina