MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali pamoja na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa 10 wa Chama hicho wakati akifunga mkutano huo uliofanyika kwa siku mbili Jijini Dodoma
RAIS Mstaafu,Jakaya Kikwete,akizungumza na viongozi mbalimbali pamoja na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa 10 wa Chama hicho uliofanyika kwa siku mbili Jijini Dodoma
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana,akizungumza na viongozi mbalimbali pamoja na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa 10 wa Chama hicho uliofanyika kwa siku mbili Jijini Dodoma
……………………….
Na Alex Sonna-DODOMA
MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi CCM) Taifa,Dkt.Rais Samia Suluhu Hassan,ametoa ahadi ya kuipanga upya Serikali ili kuendeleza Maendeleo ya nchini.
Rais Samia ameyasema hayo jijini Dodoma wakati akizungumza na viongozi mbalimbali pamoja na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa 10 wa Chama hicho wakati akifunga mkutano huo uliofanyika kwa siku mbili Jijini Dodoma.
Rais Samia amesema lengo la kufanya hivyo ni baada ya kubaini uwepo wa watu wasioendana na kasi yake.
Amesema baada ya kukamilisha kukipanga chama sasa anaelekea kuifumua serikali kwa kuwa kuna viongozi ambao hawaendani na kasi yake.
“Tumepanga safu nzuri naomba baraka zenu nikapange serikali kwa namna ambayo nitaona timu hii inaweza kwenda kutekeleza yale mliyoyasema hapa kwa vizuri.”
“Yaliyoelezwa hapa ni utekelezaji wa miaka miwili lakini katika safari yangu ya miaka miwili nahisi kabisa nina watu ambao mwendo wao hauendani na kasi yangu, tuna safari ya miaka mitatu mbele kabla hatujaenda kuwajibishwa kwa wananchi kwa hiyo miaka mitatu iliyobaki nataka serikali zote mbili zifanye kazi tutakapokwenda kwa wananchi twende tukasimame, tuwe nay a kuwaambia.”
“Tunapokwenda kwa wananchi ni wananchi wenyewe ndio wanaosema serikali iliyofanya kwao na si utamaduni wa nyuma wa serikali kuwaambia, wakati mwingine wanashangaa hiki kimefanyika wapi,”ameeleza
Aidha Rais Samia amesema kuna vijinongwa ndani ya chama vinaendelezwa na kwamba kwa mwana CCM ambaye anakijua chama na mwelekeo wa CCM “Kwa wana CCM waliotokana na chama cha mapinduzi hawawezi kufanya nongwa kuharibu chama chao lakini kuna wana CCM walioshika nyadhifa tofauti tofauti wakapitia CCM hawa wanaweza kutuharibia chama, hivyo nina toa wito kwa wanachama kuzingatia ukweli huo na tushirikiane,”amesema.
Amefafanua kuwa “Tukumbuke kushindwa kujipanga tunajipanga kushindwa, Tujipange kushinda, tunafahamu siku zote mtu anaaminiwa kwa uungwana wake, na ni kutekeleza ahadi zetu kwao.”
Hata hivyo amewaagiza watendaji wa Zanzibar na Tanzania bara washirikiane kujijenga Tanzania kwa kuheshimiana na kuzingatia mipaka ya madaraka yao.
Kwa upande wake Rais Mstaafu,Jakaya Kikwete amesema tabia ya uongo ndio inayogawa Chama cha Mapinduzi (CCM), bila sababu na kuwatengenezea viongozi msongo wa mawazo(stress) badala ya kukusanya nguvu kujenga chama.
“Mimi sina kura ila ni mzee maarufu ndani ya chama, kwanza naeleza imani hiyo na mimi naamini hivyo, Rais usikilize porojo za watu kwamba kuna kijana gani atagombea na mzee gani atagombea ni upuuzi tupu.”amesema
Aidha amesema kuwa hawazui lakini haoni mwanaCCM mwaka 2025 atakayechukua fomu labda mambo yaharibike sana kati ya sasa na wakati huo, lakini haamini hivyo, si mila yetu lakini niseme ukweli tu hapa Tanzania leo kuna mwasiasa maarufu kumshinda Samia hayupo ndani ya chama hichi hayupo nje ya chama hiki.”