Mkuu wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii, Dkt. Joyce Nyoni akizungumza wakati wa kufungua kongamano la 9 la Taasisi ya Ustawi wa Jamii jijini Dar es Salaam leo Desemba 7, 2022.
Mkuu wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii (ISW), Dkt. Joyce Nyoni akiangalia baadhi ya kazi zilizofanywa na Wanachuo waliohitimu katika taasisi ya Ustawi wa jamii.
Baadhi ya Wananchuo cha Ustawi wa Jamii wakimsikiliza mtoa mada wakati wa kongamano la 9 jijini Dar es Salaam leo Desemba 7, 2022.
************
Taasisi ya Ustawi wa Jamii wameandaa Kongamano kwaajili ya kuwanoa wanachuo waliopo, Wanaohitimu na Wahitimu wa zamani kwaajili ya kubadilishana uzoefu.
Mkuu wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii, Dkt. Joyce Nyoni akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Desemba 7, 2022 mara baada ya kufungua Kongamano hilo amesema kuwa wamekuwa wakiangalia ni ujuzi gani unahitajika kwenye soko la ajira pia ni chachu kwa wanachuo ambao wanaendelea.
Amesema kuwa Wahitimu ambao ni wafanyakazi wamekuwa wakitoa mchango mkubwakatika jamii na taasisi ikiwa ni pamoja na uitangaza.
“Wahitumu wengine wamekuwa wakianzisha Taasisi binafsi (NGO’s) ambazo zinakuwa zinatoa huduma kwa jamii, kwahiyo mhitimu wa namna hiyo anakuwa anatoa mchango wake kwa yale aliyoyafundishwa hapa Chuoni.” Amesema Dkt. Nyoni.
Kwa upande wa Mwanachuo wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii, Ally Njalila amewashukuru watoa mafunzo kwani yanawaweka katika kujua ujuzi unaohitajika katika maeneo mbalimbali ya kazi.
“Tumepata mafunzo mengi ya Msingi jambo kubwa ni kujua soko la Ajira linataka nini hivyo sisi wanachuo tunatakiwa kuyafanyia kazi yote tuliyoelekezwa.”
Akizungumzia kuhusiana na Changamoto amesema kuwa Wanafunzi wengi wamekuwa wakimaliza chuo bila kupata ajira hivyo amewasihi wanafunzi wenzake kusoma kwa bidii na kuwa na ujuzi unaohitajika kwenye soko la ajira.
Kwa upande wa Sandra Mdami ambaye ni Mwanachuo wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii, amesema kuwa Kongamano hilo limewapa ujasili wa kujiajiri au kuajiriwa na kudhubutu kufanya mambo bila kuwa na woga.
Amesema pale watakuwa na changamoto katika jamii ndio itakuwa inawapa ujasili zaidi wa kuendelea kufanya mambo mengine kwa ujasili zaidi.
“Ukiangalia watu waliofanikiwa unaona walianzia kutoka chini.”Pia amewaasa wanafunzi wenzake kuto kuthubutu kukaa na kujifungia ndani bila shughuli yeyote, amesema wajishughulishe kwaajili ya maendeleo yao na taifa kwa ujumla