Na Fredy Mgunda, Iringa.
JESHI la polisi mkoani Iringa linamshikilia
Mama mmoja anayejulikana kwa jina la Egria Ngalawa kwa tuhuma za kumtoa mimba
binti yake mwenye umri wa miaka 17 na kufukia kichanga Kwenye banda la kufugia
nguruwe lililopo nyuma ya nyumba yao katika mtaa wa Bomba mbili kata ya
Mwangata Manispaa ya Iringa.
Kwa mujibu wa mwenyekiti wa kamati
ya ulinzi na usalama wa wilaya ya Iringa ambaye ni mkuu wa wilaya ya Iringa
Mohamed Hassan Moyo alisema kuwa mtuhumiwa huyo anasadikika kutenda kosa hilo
wiki moja iliyopita kwa mujibu wa taarifa alizopokea kutoka kwa raia wema.
Moyo alisema kuwa jeshi la polisi
wilaya ya Iringa pia linamshikilia kwa mahojiano binti anayesadikiwa kutoa
mimba hiyo na kushrikiana na mama yake kufukia kichanga hicho Kwenye
banda la kufugia nguruwe.
Kiongozi huyo wa kamati ya ulinzi na
usalama Iringa akizungumza na waandishi wa habari alisema kuwa kwa mujibu wa
mahojiano Kati ya jeshi la polisi na watuhumiwa hao,inaelezwa kuwa mama wa
binti huyo aliwahi kuitwa shuleni alipokuwa akisoma binti huyo nakutaalifiwa
mwanae ni mjamzito.
Hata hivyo mama huyo amekana kuhusika
kumtoa mimba binti yake na kufukia kichanga,akieleza kuwa Amekuwa akipokea
malalamiko ya mara kwa mara ya binti yake kujihusisha kimapenzi na na wanaume
za watu mtaani hapo.
Kwa upande wake binti huyo amekana
kutoa mimba na kueleza kuwa hakuwahi kuwa na ujauzito wowote kwa kipindi hicho.
Aidha kulingana na maelezo hayo
jeshi la polisi kwa kushirikiana na ofisi ya ustawi wa jamii limeanzisha
uchunguzi wa kisayansi ili kubaini kama binti huyo anakuwa na ujauzito za siku
za hivi karibuni na uchunguzi ukikamilika hatua za kisheria zitafuata.
Tukio hilo limeibuliwa ikiwa Leo ni
siku ya kilele cha siku kumi na sita za kupinga ukatilii ambapo mkuu wa wilaya
ya Iringa Mohamed Hassan Moyo ametumia jukwaa la maadhimisho hayo yaliyofanyika
kiwilaya katika Kijiji cha Ikuvilo kukemea vitendo vya kikatili vinavyoendelea
wilaya humo huku akiwataka wananchi kupaza sauti kuwafichua watu wote
wanaojihusisha na vitendo hivyo ili hatua za kisheria zichuliwe dhidi yao.
Moyo aliwaoonya viongozi wa serikali
kuanzia ngazi ya vitongoji, vijiji na kata kuacha tabia za kumaliza kiholela
kesi za ukatilii ikiwemo ubakaji na ulawiti huku akisisitiza yeyeto
atakayebainika kufanya hivyo anafunguliwa mashtaka na serikali.